Maxime achekelea usajili wa mashine saba

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar Mecky Maxime amesema anafurahiua hatua nzuro ya usajili iliyofanywa na uongozi wa klabu hiyo kuelekea msimu mpya.

Maxime amesema hatua ya kikosi chake kuwanasa wachezaji saba ambao aliwahitaji imempa nguvu kabla ya kuanza maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.

Kagera mpaka sasa imeshawachukua washambuliaji Saadat Mohamed (Ruvu Shooting),Vitalis Mayanga(Ndanda),Hassan Mwaterema( JKT Tanzania) na Mbaraka Yusuf (Azam FC),mabeki Abdallah Mfuko(KMC) na Kiungo Mohamed Ibrahim 'MO' (Simba).

Hata hivyo kocha huyo ameitaja Simba kuwa ndio timu iliyotaka kuharibu mipango yake baada ya kuwawahi mabeki wawili aliowataka ambao ni Ibrahim Ame na David Kameta 'Duchu'.

Beki huyo na nahodha wa zamani wa Mtibwa Sugar na Taifa Stars amesema  wakati wowote kuanzia Jumatatu Agosti 17 wataanza maandalizi ya msimu mpya.

"Tulikuwa tunataka kukiboresha zaidi kikosi chetu,unaona wachezaji ambao tuliwaacha sasa lazima upate mbadala wao na hao ndio niliowahitaji kuja kuungana na kikosi changu,"amesema Maxime.

"Kuna wachezaji wawili tu ni kama niliwakosa beki Ibrahim Ame aliyesajiliwa na Duchu (David Kameta) wote walioenda Simba,kwasasa upo katika siku za mwisho kuanza maandalizi ya msimu mpya."