Dili la Tshishimbi liko hivi Simba

Saturday August 01 2020
papy pic

Pappy Tshishimbi

VYANZO vya uhakika vinadai Pappy Tshishimbi atatua Azam FC ingawa yeye amefunguka kuhusu usajili mpya akisisitiza kuwa mipango yake ya usajili haiwezi kuangalia timu moja pekee.

Licha ya hivi karibuni, klabu ya Yanga kueleza kuwa imempa siku 14 ili kuamua kama ataongeza mkataba mpya au la, mchezaji huyo raia wa DR Congo, mwenyewe amedai hajaongea na Yanga kuhusu hilo.

Katibu Mkuu wa Yanga, wakili Simon Patrick alisema; “Tulimpa siku 14, zinakwisha Jumatano ijayo, akija kusaini sawa, la hatokuja basi maana yake hataki, hivyo tutaachana naye na kuangalia mambo mengine.” Habari zinasema kwamba ameanza mazungumzo ya chinichini na Azam na huenda muda wowote ikaonekana picha yake amening’iniza uzi wa Azam.

Tshishimbi amekanusha kupewa siku 14. “Naondoka kurudi nyumbani likizo, nikiwa huko ndipo nitafanya uamuzi wa timu gani nijiunge nayo,” alisema mchezaji huyo jana alipokuwa akizungumza na Mwanaspoti.

Advertisement