VIDEO: Idris Sultan aachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na polisi kwa siku nane

Idris Sultan aachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na polisi kwa siku nane

Muktasari:

Mchekeshaji Idris Sultan ameachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakao weka bondi ya Sh 15 Milioni.

Mchekeshaji Idris Sultan ameachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakao weka bondi ya Sh 15 Milioni.

Msanii huyo alifikishwa leo Jumatano Mei 27 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kushindwa kufanya usajili wa laini ya simu ambayo ilikuwa inamilikiwa na mtu mwingine

Mei 19, 2020 Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam lilimkamata mchekeshaji huyo  ambaye  Alhamisi Mei 21, 2020 alihojiwa na kuendelea kushikiliwa.

Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime alieleza Mwananchi Digital kuwa moja ya sababu za polisi kuendelea kumshikiria msanii huyo ni kitendo chake cha kuharibu ushahidi.