Aubameyang amkuna Arteta, Arsenal ikiichakaza Everton

Muktasari:

Aubameyang ambaye kabla kujiunga na Arsenal alikuwa akiichezea Borussia Dortmund ya Ujerumani wakati wa dirisha la usajili la Januari mwaka huu,  alikuwa akiwindwa na miamba ya soka la Hispania, FC Barcelona.

Baada ya kuiongoza Arsenal kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Everton, Mikel Arteta anaamini anaweza kumshawishi mshambuliaji wake hatari Pierre-Emerick Aubameyang kuendelea kukipiga katika klabu hiyo.
Aubameyang alifunga mabao mawili katika mchezo dhidi ya Everton inayonolewa na Carlo Ancelotti  kwa sasa ametupia mabao 19 msimu huu na 60 katika michezo 95 tangu ajiunge na washika mitutu hao wa London.
"Nina furaha naye. Anafunga mabao muhimu ni nahodha, amekuwa mfano mzuri kwa kila mmoja kwa namna ambavyo
amekuwa akitekeleza majukumu yake," alisema.
Mkataba wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Gabon kuendelea kuitumikia Arsenal, unatarajiwa kumalizika mwakani, 2021.
Aubameyang ambaye kabla kujiunga na Arsenal alikuwa akiichezea Borussia Dortmund ya Ujerumani wakati wa dirisha la usajili la Januari mwaka huu,  alikuwa akiwindwa na miamba ya soka la Hispania, FC Barcelona.
"Nina kila sababu ya kuendelea kumhitaji kwenye kikosi changu kwa sababu ni mchezaji wa kiwango cha juu," aliendelea Arteta. "Nina matumaini kuwa ataendelea kuwa hapa hii ni sehemu sahihi kwake kuwa."
"Anaweza kujiona kuwa katika wakati mgumu pengine ni kutokana na matarajio makubwa aliyonayo. Anahitaji kucheza
katika  mashindano makubwa. Tunatakiwa kumsaidia kwa kufanya hivyo."
Ushindi ambao Arsenal waliupata katika mchezo dhidi ya Arsenal, umewafanya kusogea hadi nafasi ya tisa katika msimamo wa Ligi Kuu England, wakiwa na pointi 37, wameachwa kwa pointi saba na Chelsea (44)  ambao wapo katika nafasi ya nne.

ARSENAL (4-2-3-1): Leno, Bellerin, Mustafi, Luiz, Kolasinac (Saka), Ceballos (Torreria), Xhaka, Pepe, Ozil (Guendouzi), Aubameyang, Nketiah

EVERTON (4-4-2): Pickford, Sidibe,Mina, Holgate, Baines, Iwobi 6.5 (Bernard 60mins), Schneiderlin 6 (Gomes 59mins), Delph (Kean 81mins), Sigurdsson, Richarlison, Calvert-Lewin.