Molinga ampa wakati mgumu Masau Bwire

AFISA Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amejikuta katika wakati mguju baada ya mechi yao na Yanga kumalizika akizungukwa na mashabiki waliokuwa wakimtania kutokana na kichapo hicho.

Ruvu wamefungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Yanga walipata bao hilo kupitia mshambuliajia wao David Molinga akiunganisha krosi ya Ditram Nchimbi kipindi cha kwanza dakika ya 39 ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo.

Utani wa mashabiki ambao walimzonga Masau uliwalazimu Maafande kumpa ulinzi msemaji huyo mwenye mbwembwe aliyedai ni lazima waipapase Yanga hadi nje alikokuwa ameegesha gari lake.

Kipindi cha pili Ruvu Shooting walionekana kubadilika na kucheza kwa kushambulia lakini mipango yao ilionekana kugonga mwamba katika ukuta wa Yanga.

Baada ya kuona hivo kocha wao Salum Mayanga aliamua kufaya mabadiliko kwa kumtoa William Patrick na kuingia Shaban Msala.

Dakika 62 Graham Naftal alikimbia kwa kasi upande wa kulia na kupiga krosi ya chini chini na kuunganisha vizuri na Abdallahman Mussa na mpira uligonga mwamba wa juu na kudunda chini na kufanya watu kupiga kelele huku kila mmoja akiwa hajui kama ni goli au sio.

Dakika hiyohiyo Ruvu walifanya mabadiliko mengine ya kumtoa Mussa na kuingia Jamal Mnyate, walimtoa Naftal na kuingia Sadat Mohamed mabadiliko hayo yalikuwa eneo la ushambuliaji.

Dakika 67 kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi alionyeshewa kadi ya njano baada kumkanyaga Baraka Mtuwi na dakika 74 mshambuliaji wa Ruvu,  Mohamed alipewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Nchimbi.

Yanga ilifanya mabadiliko yao ya kwanza dakika 69 kwa kumtoa Molinga na kuingia Yikpe Gislain.

Katika eneo la kiungo kwenye kipindi cha pili kwa timu zote palionekana kukiwaka moto lakini upande wa Ruvu uliokuwa unaongozwa na mkongwe, Shaban Kisiga ulionekana kuwa bora zaidi kwenye kipindi hiki.

Kisiga alikuwa mwepesi katika kuisambaza mipira kwa mawinga Mnyate ambaye naye alikuwa mwepesi kupeleka mashambulizi kwa Mohamed na kuwapa presha mabeki wa Yanga.

Dakika 78 muamuzi Rafael Ikambi alisimamisha mpira na kumpa kadi ya njano beki wa Ruvu Shooting, Baraka Mtuwi, kadi hiyo alimpa licha tukio lake la kumfanyia madhambi Bernard Morrison kupita.

Yanga ilifanya mabadiliko dakika 81 kwa kumtoa Morrison na kuingia Deus Kaseke, mabadiliko hayo yalifanyika baada ya eneo la ushambuliaji la timu hiyo kupoa tangu alipotoka  Molinga.

Yanga ilitaka kupata bao la pili dakika 90 kupitia kwa mshambuliaji wao Yikpe ambaye alipiga shuti nje ya 18 na kuwa kona isiyokuwa na faida na wakati huo hio ikapigwa kona nyingine na mpira kukuana na Yikpe lakini alikosa umakini na mpira ulidakwa na kipa Makaka wa Ruvu shooting.

Yanga ilifanya mabadiliko mengine dakika 90+ kwa kumtoa Niyonzima na kuingia Said Makapu.