Jose,Pep vita ya mkwanja

Muktasari:

Ancelotti kwa sasa anam-piga mzigo huko Everton, akitua hivi karibuni kama ilivyotokea tu kwa Mourinho huko Spurs.Mourinho siku zote amekuwa akihitaji timu zenye mabosi wanaoruhusu matumizi makubwa ya pesa, huku mchezaji wake aliyem-nasa kwa pesa nyingi zaidi akiwa Paul Pogba, aliyemsa-jili akiwa Man United kwa ada ya Pauni 89.3 milioni.

JOSE Mourinho ni mtu wa matumizi. Hajawahi kuwa mtu anayejifikiria mara mbili linapokuja suala la ku-fungua pochi kufanya usajili wa maana kwenye mchezo wa soka. Jambo hilo linamfanya Mreno huyo kutumia Pauni 1.3 bilioni kwenye usajili tangu alipoanza ukocha, huku ikiwa ni zaidi ya Pauni 300 milioni kwa kocha anayemfuatia katika matumizi ya pesa ya usajili.

Mourinho amefungua pochi na kufanya matumizi makubwa zaidi akiwa Chelsea, Real Madrid na Manchester United. Kwa sasa kocha huyo anafanya kazi Tot-tenham Hotspur,bado hajaanza makeke yake ya kufungua pochi.Carlo Ancelotti ndiye anayeshika namba mbili kwa matumizi makubwa ya pesa kwenye usajili, akifanya hivyo kwenye klabu za AC Milan, Chelsea, Paris Saint-Germain, Real Madrid na Bayern Munich, lakini bado yupo nyuma kwa Pauni 300 milioni alizotumia Mourinho.

Ancelotti kwa sasa anam-piga mzigo huko Everton, akitua hivi karibuni kama ilivyotokea tu kwa Mourinho huko Spurs.Mourinho siku zote amekuwa akihitaji timu zenye mabosi wanaoruhusu matumizi makubwa ya pesa, huku mchezaji wake aliyem-nasa kwa pesa nyingi zaidi akiwa Paul Pogba, aliyemsa-jili akiwa Man United kwa ada ya Pauni 89.3 milioni.

Mreno huyo alimnasa pia Romelu Lukaku kwa Pauni 75 milioni, Fred kwa Pauni 53 milioni katika kipindi chake alichokuwa Old Trafford.Huko Chelsea kwenye vipindi vyake viwili, aliwa-nasa mastaa kama Andriy Shevchenko Pauni 40milioni, Didier Drogba Pauni 35milio-ni na Diego Costa kwa Pauni 34milioni, huko Real Madrid, aliwasajili Luka Modric kwa Pauni 31.5 milioni na Angel Di Maria kwa Pauni 30mil-ioni.

Je, Daniel Levy ataweza kummudu Mourinho kwa matumizi yake hayo?Ancelotti naye mambo yake si haba, ametumia karibu Pauni 1 bilioni (Pauni 998 milioni) hivyo kwenye usajili, huku usajili wake mkubwa ukiwa ule wa Ga-reth Bale kwa Pauni 85.3 mil-ioni alipokuwa Real Madrid na James Rodriguez Pauni 67 milioni.

Akiwa Chelsea, ndiye aliyeidhinisha usajili wa straika Fernando Torres kwa Pauni 50 milioni. Mtal-iano huyo yupo paa moja na Pep Guardiola, aliyetumia karibu Pauni 1 bilioni (Pauni 998 milioni), akipita kwenye vikosi vya Barcelona, Bayern Munich na sasa Manchester City.Nyota waliopiga pesa ndefu za Guardiola ni pamoja na Zlatan Ibrahimovic Pauni 57 milioni, Riyad Mahrez Pauni 60 milioni, Aymeric Laporte Pauni 58 milioni, Benjamin Mendy Pauni 52 milioni na John Stones Pauni 50 milioni.

Kocha Manuel Pellegrini anashika namba nne kwa matumizi makubwa, akitumia Pauni 921 milioni kwenye usajili huku usajili wake mkubwa ukiwa ule wa Cristiano Ronaldo alipom-nasa kutoka Man United kwa ada ya Pauni 80 milioni kipindi hicho akiwa Real Madrid mwaka 2009.Massimiliano Allegri ametumia Pauni 844 milioni, huku usajili wake mkubwa ni wa Ronaldo alipomnasa kutoka Madrid kwenda Ju-ventus kwa karibu Pauni 100 milioni, huku Arsene Wenger alitumia Pauni 767 milioni kwenye maisha yake ya uko-cha huku staa wake mkubwa aliyemnasa kwa pesa nyingi, akiwa Pierre-Emerick Aubameyang, wakati Roberto Mancini alitu-mia Pauni 683 mil-ioni na

 Claudio Ranieri Pauni 682 milioni. Rafa Benitez ametu-mia Pauni 577 milioni, wakati anayekamilisha 10 bora ni Unai Emery, ambaye ametumia Pauni 591 milioni, huku mche-zaji mmoja akikaribia nusu ya pesa hiyo, wakati alipomnasa Neymar kutoka Barcelona wakati huo akiwa PSG kwa ka-ribu Pauni 200 milioni.

Kwenye orodha hiyo, makocha wanne, Mourinho, Ancelotti, Ranieri na Benitez walifanya matumizi kwa kutumia pesa za bilionea Roman Abramovich, wakati makocha wengine watatu, Guardiola, Pellegrini na Man-cini walitumia mkwanja mrefu huko Man City kwa kutumia pesa za matajiri wa Abu Dhabi.

MASTAA WALIONUNULIWA KWA PESA NYINGI NA MAKOCHA HAO

1. Jose Mourinho - Pogba (Pauni 89.3milioni)2.Carlo Ancelotti - Bale (Pauni 85.3milioni)3.Pep Guardiola - Zlatan (Pauni 57milioni)4.Manuel Pellegrini - C.Ronaldo (Pauni 80milioni)5.Massimiliano Allegri - C.Ronaldo (Pauni 99.2milioni)6 Arsene Wenger - Aubameyang (Pauni 56milioni)7.Roberto Mancini - Aguero (Pauni 35milioni)8.Claudio Ranieri - Rodriguez (Pauni 38.5milioni)9.Rafa Benitez - Higuain (Pauni 34.5milioni)10.Unai Emery - Neymar (Pauni 200milion