VIDEO: Sven: Azam wanabahati kufika matuta na Simba SC

Muktasari:

Katika mchezo huo wa nusu fainali Simba ilifanikiwa kuitoa Azam kwa penalti 3-2 baada ya kumaliza dakika 90 kwa suluhu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Zanzibar. Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kufika kwao hatua ya penalti dhidi ya Azam ilikuwa ni bahati kwa wapinzani wao.

Katika mchezo huo wa nusu fainali Simba ilifanikiwa kuitoa Azam kwa penalti 3-2 baada ya kumaliza dakika 90 kwa suluhu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Sven amesema baada ya kutawala katika mchezo mzima aliamini wangeimaliza mechi hiyo ndani ya dakika 90.

Sven amesema mbinu zao bora ziliwapa shida Azam katika mechi hiyo wakitengeneza nafasi nyingi, lakini wakakosa bahati kupata mabao.

Mbelgiji huyo amesema pia wapinzani wao walikuwa na ubora wa kutofanya makosa mengi katika kudhibiti vizuri sehemu kubwa ya mashambuzi yao.

Akizungumzia mchezo wa fainali kocha huyo amesema wanaingia kujiandaa na mazingira ya fainali ngumu dhidi ya Mtibwa Sugar.

Amesema hatua ya Mtibwa kutinga fainali tena wakiwaondoa Yanga hawawezi kuiangakia mechi hiyo kwa wepesi na kwamba wataingia na mbinu za kucheza fainali.