Yanga yajipa kazi nzito Cairo

BAO la dakika 28 kutoka kwa Erick Traore limeifanya Yanga kuwa na kibarua kigumu mbele ya wenyeji wao Pyramids ya Misri katika mchezo wao wa kuwania kutinga makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga iliyopoteza mchezo wa kwanza nyumbani kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza kwa mabao 2-1 inalazimika kutumia dakika 45 za pili ili kufunga mabao zaidi ya matatu kama inataka kufanya ilichokifanya mwaka 2016 na 2018 kwa kucheza makundi ya michuano hiyo.
Kocha Zahera akimwanzisha Juma Balinya na Deus Kaseke kwenye mchezo huo sambamba na Lamine Moro aliyekuwa akiitumikia kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco United, katika dakika 45 za kwanza ilionyesha kandanda zuri.
Hata hivyo umakini mdogo katika kutumia nafasi chache ilizotengeneza imewanyima nafasi ya kupata angalau bao la kufufua matumaini ya kuvuka hatua hiyo, kabla ya wenyeji kupata bao baada ya Traore kuitanguliza Pyramids kwenye mchezo huo unaochezwa Uwanja wa Juni 30 mjini Cairo.
Licha ya kufungwa bao hilo, kipa Farouk Shikhalo amekuwa mhimili wa kuokoa mchomo mingi ya nyota wa Pyramids wanaoshiriki michuano hiyo ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo mwaka 2008.


SAFARI ya siku 85 kwa timu za Tanzania kwenye michuano ya kimataifa zilihitishwa usiku wa kuamkia leo Jumatatu baada ya wawakilishi