Majeruhi ya Neymar yatishia maisha yake ya soka

Muktasari:

Maumivu ya misuli ya paja inadaiwa kuwa ndilo tatizo kubwa zaidi linalomsumbua supastaa huyo wa Kibrazili, ambaye kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi

PARIS, UFARANSA. Mwanasoka ghali duniani, Neymar pacha zimekuwa nyingi baada ya kuumia tena, akitumia dakika 13 tu ndani ya uwanja kwenye mchezo wa kirafiki baina ya Brazil na Nigeria uliopigwa juzi Jumapili.
Beki hiyo iliyomalizika kwa sare ya 1-1, Neymar alitumia dakika 13 tu uwanjani kutolewa nje jambo linaloendeleza mlolongo wa kuumia anapokuwa kwenye kikosi hicho cha Brazil na hivyo kuigharimu klabu yake ya PSG, ambayo ililipa Pauni 198 milioni miaka miwili iliyopita kunasa huduma yake.
Neymar, ambaye alitoka na nafasi yake kuingia Philippe Coutinho, amekuwa akisumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara jambo lililomfanya acheze mechi tano tu msimu. Ameshakosa mechi nne kwenye kikosi cha PSG msimu huu, akiwa amerejea uwanjani baada ya kukosekana kwenye mechi 48 katika kipindi cha misimu miwili iliyopita.
Maumivu ya misuli ya paja inadaiwa kuwa ndilo tatizo kubwa zaidi linalomsumbua supastaa huyo wa Kibrazili, ambaye kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya alikuwa na mpango wa kurudi kwenye klabu yake ya zamani ya Barcelona kabla ya dili hilo kukwama na kuendelea kubaki Paris akiwatumia wababe wa Ligue 1.