Neymar awalipa mshahara nono marafiki zake

Muktasari:

Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona ana marafiki watatu ambao ni Gil Cebola, Jota Amancio na Carlos Henrique wakiwa pia ni wasaidizi wakuu wa Neymar, kila mmoja akitoa jukumu tofauti ndani ya 'Timu Neymar'.

Dar es Salaam. Neymar anawalipa marafiki zake karibu pauni 10,000 kwa mwezi na kuwapa nafasi ya kuingia katika sherehe za watu maarufu.

Nyota huyo wa PSG, 26 anaishi pamoja na rafiki zake katika mji mdogo wa Boshival, Paris kwenye jumba lenye thamani ya mamilioni.

Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona ana marafiki watatu ambao ni Gil Cebola, Jota Amancio na Carlos Henrique wakiwa pia ni wasaidizi wakuu wa Neymar, kila mmoja akitoa jukumu tofauti ndani ya 'Timu Neymar'.

Gil Cebola ni mpiga picha binafsi wa Neymar, Carlos Henrique anahusika na biashara za Neymar na  Amancio, mtu karibu zaidi na mshauri binafsi wa Neymar.

Amancio aliliambia gazeti la Marca Hispania "Tulikutana tukiwa na miaka 13, tangu hapo tumekuwa pamoja".

"Tuliishi na kusoma katika nyumba moja kwa miaka saba, hadi 2010 tulicheza katika timu moja" Amancio alisema.

Vile vile Cebola amezindua chapa ya mavazi, duka la tattoo na kampuni ya utengenezaji wa hafla.

 Cebola alichaguliwa na Google kupiga picha kwenye kampeni ya matangazo huko Brazil miaka ya hivi karibuni.

 

 

Huku Henrique anaonekana kuwa akili kati ya wale watatu akiangalia maslahi ya kibiashara ya Neymar.

Akiwa na thamani ya takribani pauni 110milioni, Neymar haogopi kusaidia rafiki zake kwa kuwaajiri na kuishi maisha ya kifahari.

Huku akiamini marafiki zake ndio sababu kufika mahali alipo leo.

 Santos Eduardo alifanya kazi kama mshauri binafsi wa Neymar kwa miaka sita.

Mojawapo ya kazi zake zilihusisha kutunza kadi ya benki ambayo ilifanya malipo ya marafiki wa Neymar.

"Sina shaka kuwa ni watu muhimu sana kwa Neymar, lakini nilijaribu kuwageuza kuwa msaada wa kitaalam kwa kazi ya Neymar pia” alisema Eduardo.