Uvaaji makocha Taifa Stars wazua jambo

Muktasari:

Makocha hao hawakuvaa sare zilizofanana ambapo Ndayiragije alivaa tisheti nyeupe na traki nyeusi yenye ufito mweupe pembeni, huku Mgunda juu alivaa njano na Matola ya bluu.

Dar es Salaam. Benchi la ufundi la Taifa Stars, linaongoza na kaimu kocha mkuu Etienne Ndayiragije akisaidiana na Seleman Matola na Juma Mgunda wamegeuka kivutio kwa mashabiki kwa aina ya uvaazi wao.

Makocha hao hawakuvaa sare zilizofanana ambapo Ndayiragije alivaa tisheti nyeupe na traki nyeusi yenye ufito mweupe pembeni, huku Mgunda juu alivaa njano na Matola ya bluu.

Uvaaji wao umeibua maswali kwa mashabiki ambao walifika kutazama mazoezi hayo baadhi wakihoji kama hawana yunifomu maalumu ya benchi ya ufundi.

Jezi ya Mgunda ndio ilioonekana tofauti kama za Yanga ingawa ina nembo ya TFF na bendera ya Taifa, jambo mashabiki lilikuwa kama kichekesho kwao kuona ana Uyanga.

Mashabiki wamesikika wakisema "Kwani hiyo jezi ni ya Stars ama ya Yanga, makocha wanatakiwa kuonekana nadhifu Kama TFF inavyowataka makocha wa timu za ligi kuu Bara," kauli za baadhi ya mashabiki.

Hata hivyo Mgunda ametolea ufafanuzi jambo hilo kwamba jezi yake aliovaa ina nembo za TFF, Serengeti na bendera ya Taifa.

"Watu wanaosema hawajaziona nembo za Taifa hivyo wameangalia rangi ya njano, nimevaa sahihi na nipo kwa ajili ya timu ya Taifa."