Azam FC yaondoka kwa makundi kuifuata Triangle United

Muktasari:

Timu hiyo itaondoka kwa makundi matatu kutokana na majukumu ya wachezaji wao na kocha wao mkuu, Etienne Ndayiragije anayekaimu nafasi ya ukocha katika kikosi cha Tanzania 'Taifa Stars' kuwa na mchezo dhidi ya Sudan.

Dar es Salaam. Azam FC inatarajia kuondoka nchini Jumapili hii kuelekea nchini Zimbabwe kwaajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Triangle United ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Timu hiyo itaondoka kwa makundi matatu kutokana na majukumu ya wachezaji wao na kocha wao mkuu, Etienne Ndayiragije anayekaimu nafasi ya ukocha katika kikosi cha Tanzania 'Taifa Stars' kuwa na mchezo dhidi ya Sudan.

Kundi la kwanza likiwa na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo litaondoka na kocha msaidizi Idd Nassor 'Cheche".

Kundi la pili litaondoka Septemba 23, na wachezaji watano waliopo na kikosi cha Taifa Stars ambao wataambatana na kocha mkuuz Etienne Ndayiragije.

Msafara wa mwisho utakuwa na Viongozi wakuu wa Azam Fc, wao wataungana na timu hiyo siku chache za mwisho jijini Bulawayo, Zimbabwe.

Azam itarudiana na Triangle United, Septemba 23 mchezo ambao wanahitaji matokeo ya ushindi baada ya mchezo wa nyumbani kufungwa 0-1 katika uwanja wa Azam, Complex.