Manchester United yamvalia njuga nyota Dortmund

Muktasari:

Sancho amekuwa na kiwango bora Dortmund akifunga mabao 15 katika mechi 49 alizocheza kwa kigogo hicho cha soka Ujerumani.

London, England. Winga wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho ndiye mchezaji namba moja anayewindwa na Manchester United.

Pia yumo mchezaji wa Leicester City, James Maddison ambao Kocha Ole Gunner anawataka katika usajili wa majira ya kiangazi msimu ujao.

Man United iligonga mwamba kwa Sancho (19), katika usajili wa majira ya kiangazi baada Dortmund kuweka vikwazo

Hata hivyo, Solskjaer amepania kutimiza ndoto yake kwa kuwang’oa kwa pamoja na Maddison anayecheza nafasin ya kiungo.

Sancho amekuwa na kiwango bora Dortmund akifunga mabao 15 katika mechi 49 alizocheza kwa kigogo hicho cha soka Ujerumani.

Man United inamtaja mchezaji huyo wa kimataifa wa England ni winga mwenye kipaji na uwezo wa kuipa mafanikio klabu hiyo ya Old Trafford.

Klabu hiyo ilitumia takribani Pauni150 milioni kunasa saini za wachezaji watatu Harry Maguire, Aaron Wan-Bissaka na Daniel James katika usajili wa majira ya kiangazi msimu huu.

Solskjaer anasaka wachezaji hodari wa kuziba nafasi za Romelu Lukaku na Alexis Sanchez waliojiunga na Inter Milan.

Licha ya kuwa na umri wa miaka 19, Sancho amekuwa na kiwango bora na kuzivutia klabu za Ulaya zinazotaka huduma yake.

Wakati huo huo, Man United imemalizana na kipa namba moja David de Gea kwa kumpa mkataba wa muda mrefu ambao utampa mshahara wa Pauni 375,000 kwa wiki.