CAS yampunguzia adhabu Neymar kuikosa Real Madrid

Muktasari:

Neymar alionyesha utovu wa nidhamu kufuatia penalti ambayo iliamua matokeo ya mchezo huo, dakika ya 94 katika hatua hiyo ya 16 bora ambapo iliifanya Manchester United wasonge mbele.

Paris, Ufaransa. Mshambuliaji wa Paris St-Germain, Neymar amepunguziwa adhabu ya kukosa michezo mitatu hadi mwili katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kushinda rufaa yake katika mahakama ya Usuluhishi michezoni (CAS).

Neymar mwenye umri wa miaka 27, alifungiwa na shirikisho la soka Ulaya (UEFA) baada ya kuondolewa kwa PSG wakiwa nyumbani msimu uliopita na Manchester United, Machi 6.

Neymar ataukosa mchezo dhidi ya Real Madrid na Galatasaray, lakini atarejea kuitumikia klabu yake, Oktoba 22, watacheza dhidi ya Club Bruges ya Ubelgiji.

Mbrazili huyo hakuwa sehemu ya mchezo yote miwili, nyumbani na ugenini kutokana na kushambuliwa na kwake na majeraha, alifanya utovu wa nidhamu huo kwenye mtandao wa kijamii.

"Ni aibu. Je! Anaweza kufanya nini kwa mkono, wakati amerudi?" alihoji kitendo cha mwamuzi wa mchezo huo, Damir Skomina kuona Presnel Kimpembe aliushika mpira uliopigwa na Diogo Dalot.

Hakuishia hapo, aliwashutumu waamuzi wa mchezo ule kuwa hakuna wanachojua kuhusu soka, walipaswa kuangalia hata marejeo ya picha ya Televison uwanjani pale ili kujilidhisha.

Marcus Rashford katika mchezo huo, aliifungia Manchester United penalti ile na kuihakikishia timu yake ushindi wa mabao 3-1, mchezo wa kwanza Old Trafford walipoteza kwa mabao 2-0, PSG waliondolewa na kanuni ya mabao mengi waliyopata ugenini wapinzani wao.