Diamond ana pesa nyingi ndani ya Kiba na Harmonize

Muktasari:

Kwa hatua ambayo Diamond amshapiga kwenye muziki na biashara, hatakiwi kujisononesha kwa vitu vidogo. Kuanza kulialia eti aliwekeza fedha nyingi kwa Harmonize halafu anamkimbia. Anatakiwa kuwaza kifursa. Harmonize ni fursa nzuri.

SANTURI ya ubongo iliamua kwenda kinyumenyume! Mwaka 2016 huo, ndani ya Inglewood, California, LA, ‘lilihapen’ bonge la shoo. Bad Boy Reunion Tour!
Vipi tena Bad Boy ndani ya LA? Unajua LA ni West Coast, palipo na kitovu cha Tupac Shakur, nyumbani kwa wahuni Snoop Dog, Dre, TI, Ice Cube, Naughty By Nature na wengine. Na unanyaka kuwa Bad Boy ni mabitozi wa East Coat, New York, maskani ya Notorious BIG, P Diddy, Mase na ‘kaza wa lika’. Nyakati zimebadilika!
California ndiyo jiji ambalo Tupac na Dre katika wimbo “California Love”, wanatamba ni “city of all what!” ndio, jiji lenye kila unachotaka. Ila wasitutishe, hata sisi Dar ni “city of all what!”
Kwanza California hakuna ugali wenye hamila kama Kariakoo. Hamna wahuni wenaovaa kindumbwe-ndumbwe kama watoto waliokatika ringi Chuga Town. Hawana waganga wa nguvu za kiume kila mtaa. Tunawazidi sana!
Tubaki kwenye ‘topik’, Diddy na Mase wanafungua shoo kwa ngoma kali ya 90’s, “Can’t Nobody Hold Me Down”. Shangwe kama lote. Ilikuwa siku nzuri kwa wandava wa West Coast kuburudika kwa Hip Hop soft ya East Coast. What a day!
Midamida shughuli ikabadilika! Wenye West Coast yao, Dre na Snoop si wakapanda jukwaani? Ngoma “The Next Episode” kwa hewa. Snoop na swagger zake, Dre na michano iliyonyooka, halafu lisauti la Nate Dogg, likaunguruma kuwa wao kila siku wanavuta bangi! Kudadadeki! What a day!
Sifungamani wengine walioijaza mate mic siku hiyo kama Mary J Blige, Faith Evans, 112 ambao walipata kufanya kazi Bad Boy Entertainment, mimi nipo kwenye East Coast na West Coast, pande mbili zilizokuwa na uhasama. Vifo vya Tupac na Biggie ni dhambi ya bifu hilo!
Dre na Snoop wakiwa bado jukwaani, Diddy akapanda, akanena lugha ya mataifa: “Give it up for two of my heroes, Snoop Dogg and Dr. Dre.” (Piga kelele kwa mashujaa wangu wawili, Snoop Dogg na Dr. Dre.”
Halafu Dre anaitikia: “This’s how supposed to be.” (Hivi ndivyo ilipaswa kuwa), akarudia mara mbili! Shangwe la hadhira halikuelezeka!
Diddy akamumunya risala: “We came here for healing tonight. We came here to heal some wounds and make you feel good. We can’t erase what happened. But we’re stronger, we’re better, we have way more love in our hearts and because of that, these two didn’t die in vain. Give it up for Biggie and Tupac.”
Kiswahili: Tumekuja kwa ajili ya tiba usiku wa leo. Tumekuja kutibu majeraha na kuwafanya mjisikie poa. Hatuwezi kufuta yaliyotokea. Lakini tupo imara, tupo vizuri, tuna upendo mkubwa ndani ya mioyo yetu na kwa sababu hiyo, hawa watu wawili hawajafa kilofa. Piga kelele kwa Biggie na Tupac.” Biggie na Tupac walienziwa kiasali kama Tabora!
Tuwe ‘sirias’ sasa; narudia maneno ya Dre, kuwa kilichofanyika usiku ule ndicho kilipaswa kuwa siku zote. Naam, hakukuwa na sababu ya migogoro ya Tupac na Biggie mpaka vifo vikatokea.
Kutoka Septemba 1996 Tupac alipobutuliwa risasi nne na kumsababishia kifo au Machi 1997, Biggie alipomiminiwa shaba na kuuawa, miongo mwili imekatika, Dre na Diddy akili zao hazipo tena kwenye eneo la nani anatoa ngoma kali na kutambiana mauzo. Wamekua, wanawaza nje ya sanduku!
Wameshajua kuwa kumbe hakuna hela kihivyo katika kutengeneza bifu na kugawa mashabiki, bali amani inaweza kutawala na ‘franka’ nyingi zikajaa kwenye akaunti benki. Ndio maana Dre na Snoop wanamsaidia Diddy kuandaa shoo West Coast na wao wanapanda jukwaani na kufanya kweli.
Dre na Diddy wameshaachana na akili ya kufikiria kufunikana jukwaani. Wanawaza kikubwa. Wanajiamini, wanajua wanapendwa. Dre hapotezi kuwa na ushikaji na Diddy, sanasana anaongeza. Kuna ambaye hakutaka kusikia muziki wa West Coast kwa sababu ya bifu, sasa uhasama haupo tena!
Na hapa ndipo naona kuna ‘njuluku’ nyingi za Diamond Platnumz ndani ya Ali Kiba, Harmonize, Rich Mavoko na wengine wengi. Harmonize amechomoka WCB ya Diamond na kuanzisha Konde Gang. Hii ni fursa kubwa kwa Diamond kama atawaza kibiashara, kuliko kuendekeza ‘vibifu’ ushenzi ambavyo vinaleta hasara na wakati mwingine kugharimu maisha.
Diamond badala ya kuvutana na Harmonize, angeomba naye kikao, wakanywa kahawa Hyatt Regency, The Kilimanjaro. Wakajadili nini ambacho Harmonize anataka kufanya. Kisha Diamond akaomba kuwekeza Konde Gang ili apate hisa.
Mfano, Konde Gang inapiga kazi, halafu Diamond ana hisa asilimia 30, wakati Harmonize anakuwa na asilimia 70. Hivyo, Diamond anakuwa anatazama ukuaji wa Harmonize kwa jicho chanya, kuliko mivutano isiyo na maana.
Harmonize ni mwanamuziki mzuri. Ameshathibitisha bila kuacha shaka yoyote kwamba anasafiri vizuri na dalili ni njema sana katika kesho yake. Diamond anaachaje hizo pesa ndani ya Harmonize?
Kwa hatua ambayo Diamond amshapiga kwenye muziki na biashara, hatakiwi kujisononesha kwa vitu vidogo. Kuanza kulialia eti aliwekeza fedha nyingi kwa Harmonize halafu anamkimbia. Anatakiwa kuwaza kifursa. Harmonize ni fursa nzuri.
Lazima kuacha ushamba wa kuku na mayai. Anaatamia na hataki lichukuliwe hata moja, ukimsogelea vita. Abadili mawazo na kuwaza mambo kwa namna inavyopaswa kuwa. Ujanja ni kuwa na vyanzo vingi vizuri vya mapato. Konde Gang ni chanzo kizuri kwa Diamond kama atashirikiana vizuri na Harmonize. Maisha yana utamu mwingi kama utatafuta chanya ndani ya hasi!
Mfano, badala ya kumtaka Harmonize alipe Sh500 milioni ili awe huru kuondoka WCB kama inavyodaiwa, Diamond angeweza kukubaliana na Harmonize kuwa kiasi hicho cha fidia kitumike kuijenga Konde Gang, halafu ampe hisa!
Kwa mtaji huo, Diamond angekuwa na uhakika wa kuendelea kutengeneza pesa ndani ya Harmonize siku zote za maisha yake ya kimuziki. Ukiwaza kidogo utapata kidogo, ukiwaza kikubwa utapata kikubwa!
Tuje kwa Ali Kiba! Hivi Diamond anaingiza nini kwa bifu lake na Ali Kiba? Kipi kimewahi kushindikana kwa Diamond kumwalika Ali Kiba ziara ya mbugani Serengeti, wacheze pool Singita, wapige stori za namna kila mmoja anaweza kuwekeza kwa mwenzake?
Ali Kiba ana mashabiki wengi ambao wengi wao hawataki kabisa kuamini kama Diamond ni mwanamuziki. Diamond badala ya kuchukulia hicho kitu kibinafsi, awaze kibiashara. Nini ambacho anaweza kufanya ili kutengeneza fedha ndani ya Ali Kiba?
Vivyo hivyo, Ali Kiba anapaswa kuwaza nini anapata kwa bifu ujinga na Diamond? Mbona kuna Benjamins za kutosha ndani ya Diamond? Ni wazo la namna bora ya kuishi kwa kutazama mafanikio kuliko tambo