Mabeki wa Azam, Yakub, Kangwa waishuhudia Taifa Stars, Burundi

Muktasari:

Licha ya kuwa na uraia wa tofauti wamekuwa wakijitokeza uwanjani pindi timu za Tanzania zinapocheza na wageni mechi ya kuwania kufuzu kombe la dunia, litakalopigwa 2022 nchini Qatar.

Dar es Salaam. Mabeki wa kimataifa wa Azam FC, Yakub Mohamed na Bruce Kangwa wamejitokeza katika uwanja wa Taifa katika mchezo wa Tanzania dhidi ya Burundi.

Yakub (Ghana) na Bruce (Zimbabwe) walikaa katika jukwaa la upande wa mashabiki wa Tanzania na walikiwa wakifuatilia mchezo huo ambao hadi dakika 90 zinamalizika matokeo yalikuwa 1-1 na kuongezwa dakika 30.

Wachezaji hawa wamekuwa wakijitokeza mara nyingi pindi timu za Tanzania (Klabu) zinapocheza na timu za nje.

Mabeki Yakub na Bruce msimu uliopita walikuwa wanakuja kuisapoti klabu ya simba ilipokuwa inacheza Ligi ya Mabingwa.

Tanzania na Burundi zinacheza mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Qatar 2022.