Harmonize, mkewe sarah wasamehe fungate kuishangilia Taifa Stars

Muktasari:

Mechi ya Taifa Stars na Burundi ni ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Qatar mwaka 2022.

Dar es Salaam. Mwanamuziki, Harmonize ameahirisha fungate kwa muda na kuja uwanjani kuishuhudia Taifa Stars ikicheza na Burundi.

Harmonize amefika uwanjani akiwa na mkewe Sarah raia wa Italia wamekaa jukwaa la VIP B upande ambao hupenda kukaa mashabiki wa Simba.

Harmonize na Sarah wamefunga ndoa jana Jumamosi na mke wake huyo na sherehe ilifanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Awali, hakuna mtu aliyejua Harmonizé yupo uwanjani lakini wakati wa mapumziko msanii wa nyimbo za Singeli, Msaga Sumu ndiye alimuibua.

Ni wakati anaburudisha mashabiki waliopo uwanjani,  akizunguka uwanja huku akiimba, alipofika mahali alipokuwa amekaa Harmonize alisimama na kuanza kuimba.

Wakati anaimba Harmonize naye alisimama na kuanza kucheza huku akipiga makofi.