Wachezaji Simba waingia kivingine Taifa, UD Songo wajibu

Muktasari:

Simba na UD Songo ni lazima mmoja ashinde leo ili aweze kusonga mbele baada ya mechi ya kwanza kumalizika kwa suluhu

Dar es Salaam.Wachezaji wa Simba wameingia uwanjani kwa mtindo wa aina yake wakati wakijiandaa kuivaa UD Songo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wachezaji hao wa Simba baada ya kutoka katika vyumba vya kubadilishia nguo saa 9:13, alasiri waliingia uwanjani kwa kukimbia mpaka katika kibendera cha kona ya goli lililo upande wa kaskazini mwa uwanja.

Baada ya kufika katika kibendera hiko kila mmoja alikizunguka kibendera hiko na kukizunguka hawakuingia uwanjani moja kwa moja bali yalikwenda kuingilia katika mastari wa kwanza wa eneo la penalti boksi.

Baada ya hapo waliingia uwanjani na kwenda kupasha misuli moto.

UD Songo wawajibu Simba

Wachezaji wa UD Songo ni kama wamewajibu wa Simba katika kuingia uwanjani.

Wachezaji wa UD Songo waliingia uwanjani saa 9:25 alasiri wakitokea katika vyumba vya kubadilishia nguo.

Baada ya kutoka katika vyumba vya kubadilishia nguo nao waliingia uwanjani katika eneo la kuchezea baada ya kuzunguka robo tatu ya uwanja.

Wakati wanazunguka uwanja upande wa kaskazini ambapo wachezaji wa Simba walikuwa wakipasha misuli moto walikuwa wakizomewa na mashabiki wa Simba.