Washindi Ligi Kuu kuogeshwa noti

Muktasari:

Simba ni mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kulitwaa msimu uliopita huku Yanga wakimaliza kwenye nafasi ya pili, Azam FC wakiwa wa tatu na KMC wakishika nafasi ya nne

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeahidi kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali wa Ligi Kuu msimu uliopita katika hafla itakayofanyika hivi karibuni.

Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba mpya wa udhamini wa Ligi Kuu leo, Rais wa TFF, Wallace Karia alisema kuchelewa kwa utoaji wa zawadi hizo kumetokana na majadiliano ya kumpata mdhamini mkuu wa ligi kuchukua muda mrefu.

"Ni utaratibu wa kawaida kwamba kabla msimu mpya wa ligi haujaanza, washindi mbalimbali wanapatiwa zawadi na niwahakikishie kwamba hilo litafanyika ndani ya kipindi cha wiki moja au mbili kutoka sasa.

Kwa bahati nzuri tangu tulipofanya sherehe za kufunga msimu wa 2017/2018 pale Mlimani City na Vodacoma, hakukutokea mdhamini mkuu mwingine," alisema Karia.

Zawadi zinazotarajiwa kutolewa ni ile ya bingwa wa ligi hadi mshindi wa nne, timu yenye nidhamu, kocha bora, mfungaji bora, kipa bora, mchezaji bora kijana na mchezaji bora anayechipukia