Voda waimwagia Ligi Kuu Bilioni 9

Muktasari:

Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania ilianza kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza mwaka 2002

Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, imeingia mkataba wa miaka mitatu na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kudhamini Ligi Kuu ya Tanzania Bara wenye thamani ya Shilingi 3 bilioni.

Hii ni mara ya pili kwa Vodacom kudhamini Ligi hiyo baada ya awamu ya kwanza iliyoishia msimu wa 2017/2018.

Akizungumza wakati wa hafla ya kutangaza udhamini huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi alisema wameamua kuidhamini ligi hiyo kutokana na nia yao ya kuendeleza jamii ya Kitanzania hasa soka.

"Tangu tulipoanza kudhamini takribani miaka iliyopita, tumeona hatua kubwa imepigwa kwa soka letu na vijan wengi wameweza kuendeleza vipaji vyao," alisema Hendi.

Rais wa TFF, Wallace Karia alisema udhamini huo wa Vodacom utazisaidia klabu za Ligi Kuu kumudu baadhi ya gharama za uendeshaji.

"Udhamini huu utahusa maeneo mbalimbali kama vile gharama za uendeshaji, zawadi kwa washindi wa tuzo za mwezi pamoja na washindi wa ligi na pia malipo kwa waamuzi, theluthi mbili ya fedha itakwenda kwa klabu," alisema Karia