Bocco akosekana mazoezini Simba, Aussems afichua ukweli

Muktasari:

Bocco aliumia dakika 17 katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam na nafasi yake ilichukuliwa na Clatous Chama

Dar es Salaam.Nahodha wa Simba, John Bocco amekosekana katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Gymkhana jioni ya leo.

Bocco aliumia mapema dakika 17 katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam na nafasi yake ilichukuliwa na Clatous Chama.

Baada ya mchezo huo kocha wa Simba, Patrick Aussems alisema kuumia kwa mchezaji huyo kunampa wasiwasi kuelekea katika mchezo wa marudiano dhidi ya Ud Songo.

Mwanaspoti lilifika katika mazoezi ya leo jioni na mchezaji huyo hakuwepo huku kocha Patrick Aussems akiweka wazi atamkosa Bocco katika mchezo wa marudiano dhidi UD Songo.

Aussems alisema majeraha yaliyompata Bocco yatamfanya abaki na mshambuliaji halisi mmoja Meddie Kagere kuelekea kwenye mchezo dhidi Ud Songo.

"Bocco hatakuwa nje kwa siku chache, bali atakosa hata mwezi mmoja, lakini hilo nimeshaanza kulifanyia kazi mapema," alisema Mbelgiji huyo.