Rotary Oysterbay yaandaa mbio za mbuzi Septemba 21

Muktasari:

Hii ni mara ya pili mashindano hayo kuandaliwa na klabu hiyo, mwaka jana yalifanyika na wanafunzi 42 wa vyuo vikuu mbalimbali walipata ufadhili wa masomo kutokana na fedha zilizokusanywa.

Dar es Salaam. Klabu ya Rotary Oysterbay, imeandaa mashindano ya mbio za mbuzi kuchangisha fedha za kusadia kusomesha wanafunzi wa elimu ya juu takribani 60 wasiokuwa na uwezo.
Hii ni mara ya pili mashindano hayo kuandaliwa na klabu hiyo, mwaka jana yalifanyika na wanafunzi 42 wa vyuo vikuu mbalimbali walipata ufadhili wa masomo kutokana na fedha zilizokusanywa.
Rais wa Rotary Dar es Salaam, Amish Shah, alisema mashindano hayo yatafanyika Septemba 21 na yanabebwa na maudhui ya kiarabu.
“Tunawakaribisha Watanzania katika mashindano haya ambayo tumeona watafurahi na kusaidia kuchangia fedha,”alisema Shah.