Kante hatihati kuikosa Liverpool leo UEFA Super Cup

Wednesday August 14 2019

 

London, England. Kiungo N'Golo Kante anaweza kuigharimu Chelsea katika mechi za mwanzo wa msimu, kutokana na majeruhi ya mara kwa mara.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, atakuwa nje uwanja tena baada ya kupata maumivu mapya ya mgongo.

Kocha wa Chelsea, Frank Lampard amesema Kante aliumia katika mazoezi jijini Instanbul na alikuwa na hatihati ya kucheza mechi dhidi ya Liverpool.

Kante aliingia akitokea benchi katika mchezo wa Ligi Kuu waliofungwa mabao 4-0 dhidi ya Manchester United.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, alikosa idadi kubwa mazoezi ya kujiandaa kwa msimu mpya kutokana na maumivu ya goti.

“Kante alipata maumivu kidogo katika mechi na United, ni hatari kama utaendelea kuwatumia wachezaji wa aina hii, tunahitaji kufanya uamuzi sahihi,”alisema Lampard.

Advertisement

Kocha huyo alisema anaendelea kufuatilia maendeleo ya mchezaji huyo kama atakuwa fiti kucheza mechi zijazo.

Lampard alianza vibaya msimu mpya kwenye Uwanja wa Old Trafford, kwa kipigo cha mabao manne yaliyofungwa na Marcus Rashford (mawili), Anthony Martial na kinda Daniel James.

 

Advertisement