Viongozi saba, wachezaji tisa kushiriki Michezo ya Afrika

Muktasari:

Tanzania inakwenda katika mashindano hayo ikiwa na rekodi ya kufanya vibaya  katika michezo iliyopita iliyofanyika Brazzaville, Congo

Dar es Salaam. Wanamichezo tisa na viongozi saba wataiwakilisha Tanzania katika Michezo ya Afrika (AAG) itakayoanza Jumanne ijayo nchini Morocco.

Msafara wa Tanzania umeagwa leo na kukabidhiwa bendera ya Taifa na Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini, Yusuph Singo tayari kwa safari ya Morocco huku timu hiyo itaondoka kwa mafungu.

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Neema Msitha msafara huo utaongozwa na Naibu waziri wa michezo, Juliana Shonza ambaye ataambatana na msaidizi wake.

"Kutakuwa na daktari wa timu, meneja, mkuu wa msafara ambaye tayari yuko Morocco na makocha wawili ambao wataambatana na wachezaji tisa.”

Wanamichezo hao ni  Gabriel Geay, Sarah Ramadhan, Natalia Elisante, Benjamin Kulwa, Regina Mpigachai na Ally Gulam watakuwa na kocha Mwinga Mwanjala.

Judo ni Abdulrabi Aalawi, Khamis Ally, Anangisye Kwele na kocha Innocent Malya