Mpoki anogesha mzuka mshindi wa M-Pawa

Muktasari:

Mbali na Mathias pia promosheni hiyo iliyochezeshwa jana ilishuhudia wateja wengine 339 wakivuna mkwanja wa maana kwa kuongezewa salio kwenye akaunti zao huku wengine wakishinda zawadi za simu za mkononi na muda wa maongezi.

UKISIKIA kulala masikini na kuamka tajiri ndio huku sasa baada ya mkazi wa Geita, Andrisa Mathias, kushinda kitita cha Sh15 milioni kwenye promosheni ya kuadhimisha miaka mitano ya huduma ya M-pawa.
Mbali na Mathias pia promosheni hiyo iliyochezeshwa jana ilishuhudia wateja wengine 339 wakivuna mkwanja wa maana kwa kuongezewa salio kwenye akaunti zao huku wengine wakishinda zawadi za simu za mkononi na muda wa maongezi.
Akizungumza wakati wa uchezeshaji wa promosheni hiyo jijini Dar es Salaam, Mwakilishi Mkuu wa M-PAWA kutoka CBA, Gloria Njiu alisema huduma hiyo inalenga kuwawezesha watanzania wengi wasiofikiwa na huduma za kibenki pamoja na wajasiriamali wadogo.
Alisema kuwa wanajivunia safari ya miaka mitano ya mafanikio ya huduma ya M-Pawa huku akimpongeza Mathias kwa kuondoka na mamilioni ya fedha kupitia promosheni hiyo.
Kwa upande wake, Marthias alieleza furaha yake kwa kushinda mkwanja huo na kueleza kuwa zitamsaidia katika kuendesha maisha yake. Alisema hakutegemea kushinda mamilioni hayo, lakini anashukuru na ataendelea kuwa balozi mzuri.
Naye Mwakilishi wa Vodacom, Alice Lushiku alitumia fursa hiyo kuwahimiza vijana kujiunga na huduma hiyo kwani, matokeo chanya katika maendeleo.
Droo hiyo kubwa ilishughudiwa na mabalozi wa M-Pawa, Mchezaji Mujuni Sylivester (Mpoki) na Ummy Stanslaus (Dokii) wamekuwa mstari wa mbele kuhamasisha vijana kuweka akiba.
Zawadi kwa washindi hao zitakabidhiwa leo kwenye sherehe zitakazofanyika Lugalo , Dar es Salaam.