VIDEO: Mtoto wa Banza Stone amlilia Mama Salma Kikwete

Muktasari:

Mtoto wa Banza Stone, Haji amesema anahitaji kuonana na Mama Salma Kikwete ili aweze kumuelezea shida zake.

Dar es Salaam. Miaka minne imepita tangu kifo cha mwanamuziki Ramadhani Masanja ‘Banza Stone’ kilichotokea Julai 17, 2015, mtoto wake Haji bado kilio chake kipo kwa Mama Salma Kikwete.

Haji ameiambia MCL Digital kuwa, anahitaji kuonana na mama Salma Kikwete akiwa na imani anaweza msaidia mambo mengi.

Aidha Haji ambaye wakati Banza Stone anafariki alikuwa kidato cha tatu amesema, ikifika siku ya kukumbukumbu ya kifo cha baba yake huwa anakumbuka mambo mengi sana ikiwemo maneno yake ya kumsihi asijiingize katika makundi yasiyofaa akaja kuharibikiwa na maisha.

“Mimi huwa ikifika siku kama ya leo huwa nakumbuka vitu vingi sana ambavyo baba alikuwa ananiambia kipindi yuko hai, na hata hivyo kutonana na maisha yangu ya sasa yalivyo ningependa siku niweze kuonana na Mama Salma Kikwete ili aweze kunisaidia mambo mengi,” alisema Haji Ramadhani

Banza Stone amewahi kutamba na nyimbo kadhaa zikiwemo Mtaji wa Masikini, Kumekucha, Elimu ya Mjinga, Aungurumapo Simba, Falsafa ya maisha, alifariki dunia baada kuugua kwa muda mrefu alizikwa Makaburi ya Sinza jijini Dar es Salaam.