Baba Diamond awakumbatia mama Diamond, mumewe ukumbini

Monday July 8 2019

Mwanaspoti, Baba Diamond awakumbatia, mama Diamond, mumewe ukumbini, Mwanasport, Michezo, Michezo blog

 

By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Abdul Juma baba wa msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz, ameshindwa kuzuia hisia yake na kuwakumbatia mume na mzazi mwenzie Sandra ukumbinu.

Tukio hill lilitokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu Julai 8, 2019 katika sherehe za kuzaliwa kwa mama na mchumba wa msanii huyo Tanasha Donna zilizofanyika ukumbi wa Mlimani City.

Juma alijikuta akifanya kitendo hicho pale msanii Abdul Misambano alipoimba wimbo wa 'Asu' maalum kwa ajili ya mama Diamond ambaye alieleza kipindi alichokuwa akiimba ndio walikuwa mashabiki zake.

Kibao hicho kilipoanza kupigwa kwa kutumia vyombo vya muziki vilivyokuwepo ukumbini hapo, kilimuamsha pia baba huyo kwenye kiti na kwenda kucheza na wawili hao.

Kutokana na furaha aliyokuwa nayo alienda mbali na kumkumbatia mama Sandra jambo lililosababisha watu waliokuwepo ukumbini hapo kushangalia.

Hata hivyo hakuishia kwa mama Sandra na badala yake alimwendea na mume wake Shamte wa sasa hali iliyowafanya watu kuzidi kupiga kelele za shangwe na wengine kuamkia kwenye viti.

Advertisement

Akizungumzia tukio hilo Juma alisema baada ya kufanya tukio hilo kuwa hakuogopa kwa kuwa sasa yule ni mke wa mtu.

"Kila mtu sasa hivi ana maisha yake, na hapa tupo kwa ajili ya furaha na kupongeza mzazi mwenzangu na mkwe wangu kuongeza mwaka mwingine hivyo sioni shida," alisema baba Diamond.

Advertisement