Simba yamrudisha Zana kwao kimya kimya

Muktasari:

Beki huyo alisajiliwa kwa lengo la kuziba pengo la Shomari Kapombe aliyekuwa majeruhi msimu uliopita

Dar es Salaam. Beki wa kulia wa Simba, Zana Coulibaly ameshangazwa uongozi wa Simba kumsitishia mkataba wake kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Zana ni mmoja wa wachezaji walioisaidia Simba kutetea ubingwa wake msimu uliopita pamoja na kufuzu kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika alikuwa amesaini mkataba wa miezi sita kuziba pengo la Shomari Kapombe aliyekuwa majeruhi msimu uliopita.

Zana aliwasili nchini wiki hii akitoka likizo tayari kwa maandalizi ya msimu mpya, lakini viongozi wa Simba amemwambia hawana nia ya kuendelea naye.

Zana alisema siku aliyotakiwa kurudi nchini ili kuanza maandalizi ya msimu nilifanya hivyo, lakini nashangaa viongozi wananiambia kuna mambo nimefanya ya utovu wa nidhamu.

"Nilipowauliza walianimbia ni mambo yapi niliyofanya ya utovu wa nidhamu hawakuweka wazi," alisema beki huyo.

"Kikubwa nimeamua kurudi nyumbani kama kweli watakuwa na mpango na mimi wataniita.

"Kama itashindikana hilo huku huku nyumbani nitafanya uamuzi ya kutafuta timu nyingine ambao nitaanza nayo msimu ujao," alisema Zana.

Zana wakati anarejea Tanzania alikuja kwa mbwembwe baada ya kutupa picha katika mitandao ya kijamii akionyesha anakuja Tanzania, lakini wakati anaondoka mpaka sasa amefika hakufanya hivyo.