Barcelona, Real Madrid EL Clasico ni Oktoba tu hapo

Muktasari:

Ni hivi, El Clasico ya kwanza kwenye La Liga msimu wa 2019/20 itapigwa Oktoba na ile ya marudiano itakuwa Machi mwakani baada ya ratiba mikikimikiki hiyo kutangazwa.

MADRID, HISPANIA. Sikia. Real Madrid imeshanasa silaha matata. Eden Hazard na Luka Jovic watakaokuwa pale kwenye fowadi yao. Barcelona nayo ipo kwenye harakati za kuwashusha Antoine Griezmann na Neymar huko Nou Camp.
Ushapata picha hiyo El Clasico ya msimu wa 2019/20 itakavyokuwa? Subiri, Oktoba wala sio mbali hapo, kitakapopigwa kipute cha kwanza cha El Clasico katika La Liga baada ya ratiba ya msimu mpya kutangazwa juzi Alhamisi.
Ni hivi, El Clasico ya kwanza kwenye La Liga msimu wa 2019/20 itapigwa Oktoba na ile ya marudiano itakuwa Machi mwakani baada ya ratiba mikikimikiki hiyo kutangazwa.
 Kipute cha kwanza cha El Clasico kitapigwa wikiendi ya Oktoba 27 huko uwanjani Camp Nou. Pengine hadi wakati huo, chama la Madrid litakuwa na mastaa kama Paul Pogba, Hazard na wengineo, wakati huko Barca kutakuwa na Griezmann, Neymar, Messi na Suarez, ambao wamekuwa wakiibua mjadala kwa siku za karibuni kama wataweza kucheza pamoja kwa wakati mmoja.
Mechi ya marudiano ya El Clasico itapigwa wikiendi ya Machi Mosi baada ya wote kutoka kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kwa mujibu wa ratiba ya La Liga kwa msimu wa 2019/20, vigogo hao wawili wote wataanzia ugenini, Real Madrid itaifuata Celta Vigo na Barcelona itakwenda kukipiga na Athletic Club huko Bilbao.  
Mechi za kwanza zitapigwa wikiendi ya Agosti 18, wakati ile ya Spanish Supercopa itachezwa Januari 2020. Hilo ni kwa vigogo hao wenye upinzani mkali La Liga. Lakini, Atletico Madrid nayo itaanza kampeni yake ya msimu huo mpya kwa kucheza na Getafe nyumbani, kisha itaikaribisha Real Madrid wikiendi ya Septemba 29, huku mechi yao ya marudiano itakayopigwa Bernabeu itakuwa Februari 2.  Chama hilo litaikaribisha Barcelona Desemba Mosi kabla ya kwenda Catalan kurudiana Nou Camp,