Yanga yavuna Sh 920 Mil

Saturday June 15 2019

 

By MWANDISHI WETU

HARAMBEE ya Yanga iliyoendeshwa na Kamati ya Hamasa, imevuna kiasi cha Sh 920 Milioni zikiwa ni fedha taslim na ahadi za wadau mbalimbali wa klabu hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Anthony Mavunde alisema kwa shughuli iliyofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee leo, walikusanya fedha taslimu Sh 263 milioni, huku zile za awali zikiwa Sh252 milioni na fedha hizi zikichanganywa pamoja na ahadi zote zinatoa jumla ya Sh 920 milioni.
Lengo la Kamati hiyo ni kukusanya Sh 1.5 bilioni kwa nia ya kusaidia usajili wa klabu hiyo kwa kikosi cha msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.
"Kwa hakika tunajivunia kwa hili lililofanywa na Wanayanga na wale wanaotaka kuendelea kuichangia wanakaribishwa kwa vile Yanga bado inahitaji fedha kwa maendeleo ya klabu hiyo," alisema Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla.

Advertisement