Nadal abeba taji la 12 French Open

Muktasari:

Taji hilo ni la 18 katika historia yake ya mataji makubwa aliyobeba kwenye tenisi, huku akiwa amezidiwa mawili tu na Swidishi, Roder Federer, ambaye alimshinda kwenye nusu fainali ya mashindano hayo ya French Open

PARIS, UFARANSA. Rafael Nadal hakamatiki huko kwenye mashindano ya French Open baada ya kumchapa Dominic Thiem na kubeba taji la 12 la mashindano hayo kwa upande wa wanaume.
Mhispaniola huyo alishinda taji hilo la Grand Slam kwa mwaka wa tatu mfululizo huko Roland Garros baada ya kumtandika Thiem kwa 6-3 5-7 6-1 6-1 katika fainali iliyokuwa na upinzani mkali.
Lakini, taji hilo ni la 18 katika historia yake ya mataji makubwa aliyobeba kwenye tenisi, huku akiwa amezidiwa mawili tu na Swidishi, Roder Federer, ambaye alimshinda kwenye nusu fainali ya mashindano hayo ya French Open. Mkali wa Serbia na namba moja duniani katika chati za ubora za mchezo huo, Novak Djokovic. Kuhusu French Open, Nadal amekuwa mchezaji wa kwanza kushinda taji hilo mara 12.
Thiem, ambaye anashika namba nne kwenye viwango vya dunia vya mchezo huo, alipoteza fainali yake ya pili ya Grand Slam wakati alipofungwa kwenye seti tatu dhidi ya Nadal mwaka jana.
Tano bora ya wakali wanaoongoza kwa kubeba Gland Slam kwa upande wa wanaume, Federer anaoongoza akiwa na mataji 20, anafuatia Nadal mataji 18, kisha Djokovic mataji 15, Pete Sampras mwenye mataji 14 na Roy Emerson amebeba mataji 12.