Mwadui, Kagera Sugar zabaki Ligi Kuu

Muktasari:

Mwadui na Kagera Sugar walifikia hatua hiyo baada ya kuwa na matokeo mabaya msimu wa Ligi Kuu uliomalizika kwa kukusanya pointi 44 kila mmoja hivyo kulazimika kucheza mechi hizo na timu za Daraja la Kwanza.

MWADUI FC na Kagera Sugar, zimebaki kwenye ligi msimu ujao baada ya kushinda mechi zao za mchujo dhidi ya wapinzani wao.

Mwadui na Kagera Sugar walifikia hatua hiyo baada ya kuwa na matokeo mabaya msimu wa Ligi Kuu uliomalizika kwa kukusanya pointi 44 kila mmoja hivyo kulazimika kucheza mechi hizo na timu za Daraja la Kwanza.

Kagera Sugar wlaipangwa kucheza na Pamba FC ya jijini Mwanza mabapo mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka suluhu sawa na Mwadui ambao pia walisuluhu na Geita Gold, mechi hizo zilichezwa ugenini.

Mechi za marudiano timu hizo za Ligi Kuu zote zimebaki kwa kushinda, Mwadui iliikaribisha Geit Gold na kushind abao 2-1 wakati Kagera Sugar ikishinda uwanja wao wa nyumbani wa Kaitaba bao 2-0.

Mshambuliaji wa Mwadui FC, Salim Aiyee aliyefunga mabao yote mawili ndiye aliyeibakiza timu yake msimu ujao wakati bao pekee la Geita lilifungwa na Baraka Jerome.

Ally Ramadhan alianza kuifungia bao Kagera Sugar dakika ya 50 huku Japhet Makalai akihitimisha bao la pili dakika ya 79.

Mchezo wa Kagera Sugar na Pamba ulikuwa na presha kubwa ambapo kulikuwa na vituko vya hapa na pale nje na ndani ya uwanja huku wachezaji walicheza kwa kukamiana.

Kwa matokeo hayo, ambayo yalikuwa yakihitaji timu mbili kupanda daraja yanafikisha timu 20 msimu ujao baada ya Namungo FC na Polisi Tanzania kupanda daraja moja kwa moja.