Eti! Hakuna msanii anayemfikia Juma Nature kwa fedha, Mali

Sunday June 2 2019

Mwanaspoti, Hakuna, msanii, anayemfikia, Juma Nature, fedha, Mali

 

By Rhobi Chacha

Dar es Salaam. Mwanamuzi Juma Nature amedai yeye ana fedha na mali nyingi na hakuna msanii yeyote wa Tanzania anayemfikia.

Nature amesema yeye sio kama baadhi ya wasanii wenye tabia ya kujisifia kwa kutangaza utajiri kwa kuonyesha baadhi ya mali zao.

Nature amesema kitendo hicho kinachofanywa na baadhi ya wasanii ni ulimbukeni na wakati mwingine utakuwa asilimia kubwa mali zinakuwa siyo zao.

 "Mimi watu wanadhani nimefulia sasa, niwaambie tu mimi sijafulia na nina pesa nyingi kuliko msanii yeyote hapa Tanzania, watu wanachukuliana poa tu.

"Kwanza sasa hivi watu wameshashutka wasanii asilimia kubwa wanafeki maisha wanayoishi, hivyo hata baadhi yao wanaotangaza mali zao zinakuwa sio zaoa."

 Juma Nature aliwahi kutamba na albamu ya Ugali katika album hiyo kulikuwa na nyimbo Sitaki demu, Ugali, Salio la vesi, Jela, Aah wapi, Umoja wa Tanzania (feat. Prof. Jay), Hali ngumu, Sitaki demu RMX na Inaniuma sana.

Advertisement

Advertisement