VIDEO: Mabango ya sherehe za ubingwa wa Simba yatelekezwa Uwanja wa Taifa

Muktasari:

Mechi ililazimika kuchezwa mapema kuanza saa 9:00 alasiri ili kupata muda wa kutosha sherehe na mambo mengine yote kufanyika uwanjani hapo.

Dar es Salaam. Shirikisho la soka Tanzania TFF liliandaa mabango ya kupamba sherehe za ubingwa Ligi Kuu Bara wa Simba, ghafla jambo hilo lililayeyuka na kufanya mashabiki kuondoka kwa kinyongo uwanjani.

Baada ya kumalizika mechi mashabiki walikaa mkao wa kusubiria kombe, lakini wakajikuta timu zinaondoka ndipo wakajua kwamba jambo hilo limegonga mwamba.

Katika pitapita Mwanaspoti lilikumbana na mabango yaliandaliwa maalum kwaajili ya kukabidhiwa kwa kombe hilo yakiwa yametelezwa nje.

Hata hivyo uwanjani hapo wakati mashabiki wakiwa wanasubiri kuona kombe hilo, haikutoka taarifa yoyote kwamba sherehe hizo hazitafanyika.

Mwanaspoti lilishuhudia mashabiki hao wakilalama kutoonekana kwa kombe ambalo waliltegemea kuona wachezaji wao wakikabidhiwa katika uwanja wa Taifa.

Katika kuhakikisha hilo linawezekana na kufanyika kwa Simba kupewa zawadi zao na sherehe za ubingwa.

Mechi ililazimika kuchezwa mapema kuanza saa 9:00 alasiri ili kupata muda wa kutosha sherehe na mambo mengine yote kufanyika uwanjani hapo.

Wakati mchezo huo ukiwa unaendelea yalitoka maamuzi kuwa tukio la kakabiziwa ubingwa na sherehe zitafanyika katika mchezo ujao dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mechi ya Simba na Mtibwa Sugar ndio itakuwa ya mwisho msimu huu ambayo itapigwa Mei 28, siku ya mwisho kwa timu zote kucheza michezo ya mwisho.

Katika mchezo wa kwanza kati ya wenyeji Simba dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa Uwanja wa Uhuru mabingwa walishinda 3-0.