MFALME: Lionel Messi amfunika Ronaldo kwa mataji

Muktasari:

Pamoja na rekodi hiyo pia rekodi nyingine ni ya kuwa mfungaji mwenye mabao katika mashindano yote, mabao 324 katika mechi 308 sawa na wastani wa 1.5 kwa kila mechi. Bao moja zaidi na mechi 433 katika rekodi ya siku za nyuma iliyokuwa ikishikiliwa na Raul.

Katika toleo lililopita mwandishi Luca Caioli alichambua tukio la Ronaldo kuiwezesha Real Madrid kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya huku kocha wake Zinedine Zidane akisifia kiwango cha mchezaji huyo ambaye pia alikuwa na rekodi nzuri ya mabao katika ligi hiyo. Endelea…
“Wewe uko katika kiwango cha juu,’’ Zidane alisikika akimwambia wakati wa kufurahia ushindi huo. Na huo ni ukweli walau unapozungumzia mabao aliyoyafunga katika mashindano hayo. Ronaldo alikuwa ndiye mfungaji bora na mabao yake 16 karibu zaidi ya nusu ya aliyofunga straika wa Bayern Munich, Robert Lewandowski aliyeshika nafasi ya pili.
Kwa Barca, Suarez aliibuka mfungaji bora na kutwaa kiatu cha dhahabu katika La Liga na hivyo kuibeba tuzo ambayo msimu uliopita ilichukuliwa na Ronaldo lakini kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya hakuna aliyemsogelea Ronaldo.
Kwa mtazamo wa Ronaldo hilo ndilo lililokuwa na maana kubwa, “Barca kubeba La Liga na Kombe la Mfalme hainisumbui mimi kwa sababu najua tunaposhinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya hadhi yake ni kubwa zaidi kuliko hayo mataji mawili.”
“Kuna wachezaji wengi mastaa ambao hawakuwahi kushinda taji hili japo mara moja, kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya ni ndoto, nakwambia kutoka ndani ya moyo, siwezi kulibadili taji hili na chochote,’’ alisema Ronaldo siku chache kabla ya mechi ya fainali.
Kwa kulitwaa taji hilo mjini Milan mwaka 2016, Real Madrid wakawa wamefanikiwa kupunguza majanga ya msimu wa hovyo yaliyokuwa yakiwakabili katika siku za karibuni ikiwamo wakati wakiwa chini ya Kocha Jose Mourinho.
Msimu ulianza na Rafa Benitez ambaye alikabidhiwa jahazi akichukua nafasi ya Carlo Aneclotti na haraka ikabainika kwamba hakukuwa na maelewano mazuri kati ya kocha na mchezaji staa.
Utata huo ikawa sababu ya Benitez kuondoka mapema na kumpisha Zidane muda mfupi baada ya mapumziko ya Krismasi, kuanzia hapo timu ikabadilika ghafla na kuanza kupata mafanikio na hatimaye kufikia hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ronaldo kuwa mfungaji mwenye mabao mengi wa Real Madrid katika La Liga, mabao 231.
Pamoja na rekodi hiyo pia rekodi nyingine ni ya kuwa mfungaji mwenye mabao katika mashindano yote, mabao 324 katika mechi 308 sawa na wastani wa 1.5 kwa kila mechi. Bao moja zaidi na mechi 433 katika rekodi ya siku za nyuma iliyokuwa ikishikiliwa na Raul.
Mlinganio wa misimu kadhaa ulitoa wazo moja tu kuhusu wachezaji hawa wawili, ‘mafanikio makubwa. Lakini pia ina maana kubwa kuangalia mataji mangapi wachezaji hawa wawili wameyashinda na klabu zao.
Messi anaongoza kwa mbali, hasa kwa kuwa amefaidika na miaka bora na ya mafanikio ya Barca, ameshinda mataji manane (sasa 10) ya La Liga, sita ya Spanish Super Cup, manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, manne (sasa sita)ya mfalme, matatu ya Uefa Super Cup, na matatu ya klabu ya dunia. Yote hayo na Barcelona.
Ronaldo anachuana vikali na Messi kwa mataji, ameshinda mataji na klabu tatu za Sporting Lisbon, Manchester United na Real Madrid, ana mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya matatu (sasa matano), mawili (sasa manne) ya klabu ya dunia, moja la FA, mawili ya Kombe la Ligi, mawili ya Ngao ya Jamii, mawili ya Ligi Kuu England, La Liga moja (sasa mawili), mawili ya Kombe la Mfalme, moja (sasa matatu) ya Uefa Super Cup na moja (sasa mawili) ya Spanish Super Cup. Nje ya mabano ni rekodi za kufikia mwaka 2017, kilipoandikwa kitabu hiki ambapo rekodi ya Messi-Ronaldo ya mataji ilikuwa 29 kwa 18.
Kufikia hapo, Messi alikuwa amemuacha mbali Ronaldo kwa mataji