Mashabiki wa Simba walisusa Kombe Uwanja Taifa

Muktasari:

Simba inasherehekea sherehe za ubingwa leo Jumamosi ambapo watakabidhiwa na Waziri Mambo ya Ndani, Kangi Lugola.

Dar es Salaam.Mashabiki wachache wamejitokeza uwanja wa Taifa, kuishudia Simba ikicheza na Biashara United kabla ya kukabidhiwa ubingwa wao wa 20 wa Ligi Kuu Bara.
Tofauti na msimu uliopita uwanja ulijaa mashabiki, leo mchezo ulianza mapema saa 9 alasiri huku mvua ikinyesha katika maeneo  inaendelea jijini Dar es Salaam.
Simba inasherehekea sherehe za ubingwa leo Jumamosi watakabidhiwa na Waziri Mambo ya Ndani, Kangi Lugola.
Simba ambayo tayari imetwaa ubingwa wa ligi kuu Bara kwa mara ya pili mfululizo, itakabidhiwa kombe lao baada ya mechi hiyo kumalizika ambapo hadi dakika 45 za mwanzo timu hizo zilitoka sare ya bao moja.
Mechi hiyo inachezwa uwanja wa Taifa ambapo uwanja huo umekuwa na maji mengi yanayopekea wachezaji kushindwa kucheza soka safi kwani mara nyingi wanateleza na mpira kuwaponyoka.
Biashara United ambayo ipo chini ya kocha Said Amri 'Stam' ndiyo ilianza kutikisa nyavu za wenyeji wao dakika ya 13 kupitia Innocent Edwin ingawa dakika tatu baadaye Clatous Chama alijibu mapigo kwa kusawazisha dakika ya 16.
Mechi hiyo kwa Simba hawana cha kupoteza kuliko Biashara United ambao wanatengeneza nafasi nzuri ya kubaki kwenye ligi kwani katika msimamo wanashika nafasi ya 16 wakiwa na pointi 43 sawa na Prisons wakitofautina idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.