Kisa BSS: Wimbo mpya wa Harmornize wazua zogo mtandaoni

Muktasari:

Mwanamuziki huyo aliwahi kukoselewa na majaji wa shindano la BSS, Madame Ritha, Salama Jabir na Master J kuwa hajui kuimba.

Dar es Salaam. Wimbo mpya wa ‘Never give up’ wa mwanamuziki Hamornize umezua mjadala katika mtandao wa kijamii baada ya kutuma kipande cha video kilichomuonyesha akikosolewa na majaji wa shindano la kusaka vipaji vya wanamuziki ‘BSS’.

Hamornize anayeunda kundi la Wasafi Classic (WCB) ametoa wimbo huo na kuweka kipande hicho chake cha kuambiwa hajui kuimba katika shindano la BSS, kimesababisha watu wengi kudhani ni dogo kwa majaji Salama Jabiri, Madame Ritha na Master J.

Kutokana na utata huo Hamorinize katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ameamua kuweka wazi kwa suala hilo kwa kuandika hivi: Naomba kuliweka hili suala sawa.!! Maana ya kuiweka hii Clip katika wimbo wangu sio kuwasuta #BSS ama kuwaonyesha now nimefanikiwa kama baadhi ya watu wanavyo itafsili hapana mie ndiokwanza ninaanza na ninaamini ninasafari ndefu sana...!!!

Lengo ni kuwaonyesha vijana wenzangu kuwa kwenye hii dunia kilakitu kinawezekana haijalishi kuwa unakatishwa tamaa unadharaulika wanakunyanyapaa isikufanye ujione wewe sio wathamani na hata kuzikaatisha ndoto zako na hakuna elimu iliyobora kama ya kumuonyesha mtu mfano ulio hai najua hii Video imewapa na inawapa watu wengi sana Nguvu mpaya na kuwafanya waendele..!!! Nikiwepo mimi mwenyewe nikiitazama hii inanipa nguvu pale ninapokaribia kukata tamaa....!!!

Hivyo niseme Nawapenda na kuwaheshimu Sanaa...!!!! #BSS @mspaulsen x @masterjtz x @ecejay x naamini wamesaidia vijana wengi sanaa...!!! Kwa upende wao nisingependezewa kuona hii inatumika kuwavunjia heshima na kuyafuta mengi mazuri waliyo yafanya ???? Naa kazi zao zinalawama kubwa mno fikiria tuu kuchagua watu mmoja kwenye 1m sio kazi rahisi Mungu awabariki sanaaa tuendelee kuikuza sanaa ya Tanzania Wenda wangenisifia nisingefika leo nisingesimama mbele yenu na mkajivunia ???? Brand new #NeverGiveUp out now link in my Bio