Niyonzima kawa mtamu kinoma Sevilla wamemkoma

Thursday May 23 2019

Mwanaspoti, Michezo, Michezo blog, Niyonzima, mtamu,Sevilla, Simba, Sportpesa

 

By Thomas Ng'itu

Dar es Salaam. Achana na matokeo Simba kuchapwa 5-4 na Sevilla, utamu ulikuwa pale kati katika eneo la kiungo Simba kulikuwa na starehe ya aina yake baada ya kiungo Haruna Niyonzima kufanya madoido yake.

Niyonzima alionyesha uwezo mkubwa katika kumiliki mpira kugeuka kuwa nyota katika eneo hilo la kiungo.

Simba walimuanzisha Niyonzima, Jonas Mkude na Clatous Chama katika eneo la kiungo, huku Sevilla wakiwaanzisha Ever Banega, Quincy Gomes na Roque Sema.

Chenga za Niyonzima ziligeuka kuwa kivutio kwa mashabiki wa Simba ambao walikuwa wamejitokeza uwanjani.

Viungo wa Simba waliweza kumiliki mpira kwa uwezo mkubwa na kuwafanya viungo wa sevila wakihangaika.

Dakika 63 Niyonzima alitoka na nafasi yake ilichukuliwa na Hassan Dilunga ili kwenda kuongeza nguvu zaidi katika eneo hilo licha ya kwamba walikuwa vizuri katika kushambulia.

Advertisement

Advertisement