Bocco, Kagere waitungua Sevilla, VVIP kumenoga Taifa

Thursday May 23 2019

Bocco, Kagere, Simba, waitungua, Sevilla, Mwanaspoti, Michezo, Michezo blog, Mwanasport

 

By Thobias Sebastian

Dar es Salaam. Mabao mawili ya nahodha John Bocco na moja la Meddie Kagere limeifanya Simba kwenda mapumziko wakiwa mbele magoli 3-1 dhidi ya Sevilla katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Bocco alifunga mabao mawili dakika 8, 32 akimalizia kazi nzuri ya Kagere kabla ya Mnyarwanda huyo kinara wa mabao wa Ligi Kuu Bara kufunga bao la pili dakika 14, Sevilla imepata bao dakika 23, kupitia Wissam Been Yedder.

Simba imetawala sehemu kubwa ya mchezo huo wakiwa hatari zaidi kila wanapofika langoni mwa Wahispania hao waliokuwa wakicheza taratibu.

Awali uongozi wa Simba katika kuhakikisha mambo yanakwenda sawa haswa kwa mashabiki wao waliojitokeza uwanjani waliweka utaratibu maalumu.

Mashabiki walipata tiketi za Platinumz wanakwenda kukutana Serena Hoteli na baada ya hapo wanachukuliwa na Mabasi maalumu huku wakiwa kwenye msafara unaongozwa na polisi.

Mashabiki wengine waliojitokeza Uwanjani ni wale ambao wanapesa mualiko maalumu na hukaa kwenye jukwaa kuu.

Advertisement

Mashabiki wale wa patimanumz na ambao walikuwa na mualiko maalumu walikuwa wakipomelewa na wasichana maalumu warembo na kuwaelekeza kwa kukaa.

Baada ya hapo ulipifika muda wa kupata futari walichukuliwa na wale wale wasichana Warembo na kuwaeleza chumba ambacho kiliandaliwa kwa ajili ya futari.

Ukitoka katika chumba cha futari ilikuwa unakutan na mdada mwingine mrembo ambaye alikuwa karibu na fliji ambalo lilikuwa na maji na juisi ambayo ulikuwa unapatiwa kimoja wapo.

Wakati unarudi kukaa katika kiti chako unakutana tena na warembo ambao walikuwa wanakuelekeza tena kwa kukaa.

 

Advertisement