Wachezaji Sevilla FC waonja joto ya foleni Dar es Salaam

Muktasari:

Sevilla FC itacheza mechi ya maalum ya kirafiki dhidi ya Simba iliyoandaliwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa Tanzania.

Dar es Salaam.  Msafara wa timu ya Sevilla FC umeonja hadha ya foleni ya Jiji la Dar es Salaam baada ya kusota  kwa takribani saa moja kurejea hotelini mara baada ya kumaliza mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa.

Sevilla FC itacheza mechi ya maalum ya kirafiki dhidi ya Simba iliyoandaliwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa Tanzania.

Msafara wa timu ya Sevilla ambayo Mei 23 usiku itacheza mechi maalum ya kirafiki idhidin ya klabu ya Simba kwenye uwanja wa Taifa, ulituamia njia ya Kilwa ana kulazimika kupitia barabara ya pembeni ulipofika kwenye mzunguko wa Jitegemee.

Pamoja na kutumia askari wa usalama barabarani (muongoza msafara), msafara huo ulikwamamara baada ya kufika Polisi Ufundi na kulazimika kupita eneo la katikati ya barabara ambalo hakina lami mpaka kwenye mzunguko wa barabara ya kwenda Shimo la Udongo.

Msongamamo wa magari ulikuwa mkubwa sana na iliwafanya askari wa Barabarani kutumia maarifa ya ziada ili kuuwezesha msafara huo kupenya katika msongamano mkubwa wa magari.

Mbali ya wachezaji, hadha hiyo pia iliwakumba viongozi wa kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa iliyoandaa mechi hiyo.

Msafara huo ulipofika eneo la mzunguko wa BP ulianza kupata nafuu kutokana na kupata nafuu kutokana na magari ya foleni kuanza kupungua.