Rage: Yanga wakajipange upya msimu ujao

Monday May 20 2019

Mwanaspoti, michezo, Michezo blog, Rage, Yanga, wakajipange, msimu ujao, Simba, Mwanasport

 

By Imani Makongoro

Dar es Salaam.Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Ismail Aden Rage amewakebehi watani zao Yanga akiwataka wafikirie kutoa maji yaliyojaa klabuni kwao siyo ubingwa msimu huu wameshaukosa.

Rage amekwenda mbali zaidi akiwatania Yanga kuwa kipindi hiki ambacho mvua inaendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, wafikirie kutoa maji yatakayojaa klabuni na si ubingwa.

Huku akicheka, Rage alisema ubingwa huko wazi kwa Simba na kusisitiza kuwa hata utokee muujiza Yanga hawawezi kupindua meza.

"Ubingwa huko wazi kwa Simba, watani zetu Yanga labda kwa msimu ujao, warudi wakajaipange upya, lakini sio kuota ubingwa wa msimu huu," alisema Rage.

Timu hiyo ambayo msimu uliopita ilitwaa ubingwa, ilifanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na kufika robo fainali na kutolewa na TP Mazembe ya DR Congo.

Advertisement