Simba yaitekenya Ndanda mabao 2-0 ikibakiza pointi moja kutwaa ubingwa

Sunday May 19 2019

 

By Thobias Sebastian

Dar es Salaam. Timu ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa leo Jumapili kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba yaliwekwa wavuni na Meddie Kagere dakika 5 na 11 kipindi cha kwanza na kuifanya timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi kufikisha alama 88 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Kipindi cha kwanza kimemalizika katika mechi ya Simba dhidi ya Ndanda huku wenyeji wakitoka kifua mbele.

Simba walipata mabao 2-0 ndani ya dakika 15, za mwanzo yote mawili yaliyofungwa na Maddie Kagere.

Mabao hayo ya Kagere yanakuwa 22, msimu huu kwake akiifungia timu yake ya Simba iliyomsajili kutokea Gor Mahia ya Kenya kabla ya kuanza kwa msimu huu.

Mabao hayo mawili ya Kagere anaweka rekodi ya kuifungia Simba mabao 36, tangu alipojiunga nayo katika mashindano yote.

Advertisement

Kipindi cha kwanza Simba walionekana kushambulia mara kwa mara kuliko wapinzani wao Ndanda.

Ndanda walionekana kufanya mashambulizi machache na ya kushtukuza ambayo Simba hawakuwa hatari sana.

Kwa upande wa Simba walionekana kufanya mashambulizi kuliko Ndanda na mengine yakionekana kuwa ya hatari.

 

Advertisement