Mwanri aonyesha umahiri wake wa soka uzinduzi Copa Umiseta

Sunday May 19 2019

 

By Imani Makongoro

Dar es Salaam.Baada ya kutamba kwa maneno kuwa enzi zake alikuwa anapiga chenga wachezaji wenzake mpaka anakalia mpira, anauwezo wa kufunga kama mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Italia, Gennaro Gattuso na kudaka kama kipa nyota wa zamani wa Nigeria, Emmanuel Okala, Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amedhihirisha ubora wake kwa kupiga danadana na kufunga penati.

Mwanri  alionyesha makali yake wakati wa uzinduzi wa michezo ya shule za sekondari (Copa Umiseta) kwa kufunga penati na kupiga danadana kwa kutimia mguu wake wa kushoto kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi na kuwapagawisha mashabiki wa soka waliohudhuria uzinduzi huo.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, Mwanri alisemakuwa michezo hiyo ni muhimu na ni sehemu muhimu katika malezi ya ya vijana ikiwa pamoja na afya.

“Natoa shukrani  na pongezi za dhati kwa Kampuni ya Coca-Cola kwa kuwa jicho kwenye soka la vijana nchini Tanzania. Uwekezaji wenu katika soka kwa zaidi ya miaka mitatu sasa umekuwa kichocheo cha maendeleo ya vipaji kwa klabu zetu za ndani na pia kwa timu yetu ya Taifa Stars,” alisema Mwanri.

Meneja Mauzo na Masoko wa Nyanza Bottling Company Ltd, Samwel Makenge alisema kuwa mbali ya kucheza michezo tofauti, mashindani ya Copa Umiseta ya mwaka huu ni sehemu ya kampeni, wanafuzi wa shule za sekondari wataelimishwa na kupewa mafunzo ya namna ya kuileta jamii karibu ili itambue umuhimu wa hifadhi ya mazingira yetu kupitia dhana ya urejeshaji.

Zawadi nyingine ni pamoja na mashine moja ya kudurufu, projekta mbili, kompyuta mpakato 108, kompyuta 11, vishikwambi(Tablets) 108, saa 12,jezi 1176 na mipira 360 kwa washindi wa kila kipengele katika kampeni hiyo.

Advertisement

Mwisho…

Pix 1

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri akipiga penati kuashiria uzinduzi wa michuano ya Copa Coca-Cola UMISSETA kwa mkoa wa Tabora wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika jana mkoani humo.

Pix 2

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri akipiga penati kuashiria uzinduzi wa michuano ya Copa Coca-Cola UMISSETA kwa mkoa wa Tabora wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika jana mkoani humo.

Advertisement