Thursday May 16 2019

WACHEZAJI wa Timu ya Taifa ya Tanzania ya mchezo wa gofu wameanza kuingiwa na mchecheto kuchukuliwa nafasi zao katika timu hiyo na wachezaji chipukizi wanaoibuka hivi sasa.

Wasiwasi huo umeanza kuingiwa baada ya wachezaji chipukizi kushiriki katika mashindano ya kutafuta wachezaji watakaowakilisha Tanzania katika mashindano ya Kanda ya Nne ya Afrika nchini Burundi juni mwaka huu.

Katika mashindano hayo, chipukizi hao waliweza kuonyesha viwango cha hali ya juu siku zote nne za mashindano hali iliyofanya wachezaji wazoefu wa timu ya taifa wacheze kwa uangalifu mkubwa kuhofia kushindwa. Mashindano hayo ya kufuzu kuchezea Timu ya Taifa yalichezewa kwenye viwanja vya Kili gofu,Moshi Gymkhana, TPC na Arusha Gymkhna.

Katika mashindano hayo chipukizi Isiaka Daudi anayechezea klabu ya Lugalo alikuwa ni miongoni aliyekuwa anawasumbua wachezaji wa timu ya taifa akiwemo Victor Joseph,Abasi Adamu na Frank Mcharo.

Daudi katika mashindano hayo alishika nafasi ya tano,huku nafasi ya kwanza mpaka ya nne ikichukuliwa na Victor Joseph,Frank Mcharo, Abas Adamu na Richard Mtweve.

Akizungumzia kuhusiana na chipukizi hao ,naodha wa timu ya taifa ya Tanzania Victor Joseph, alisema kutokana na viwango walivyoonyesha Daudi na Juma Likuli alidai wana uwezo kuchezea timu ya taifa

Advertisement

“Tumecheza pamoja tangu mwanzo na tulikuwa tunashindana hasa na tungeweza kuwadharau nafasi za juu zingechukuliwa na chipukizi hawa,” alisema Joseph

Akizungumzia maendeleo yake Daudi alisema klabu ya gofu ya Lugalo imeweza kumfanya aonekane ana uwezo mzuri wa uchezaji kutokana na klabu hiyo kuwadaa vizuri kwa program ya ufundisha gofu kwa vijana waliyo nayo.

Advertisement