Kiungo wa timu ya Taifa ya Burundi afia uwanjani Eswatini

Thursday April 25 2019

Mwanaspoti, Mwanasport, Kiungo, timu ya Taifa, Burundi, afia, uwanjani, Eswatini

 

Dar es Salaam. Kiungo Mrundi Papy Faty amefariki jioni ya leo baada ya kuanguka akiwa uwanjani aliitumikia klabu yake mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe amethibitisha.

Taarifa kutoka nchini Eswatini zinasema Faty amekutwa na umauti wakati akiitumikia timu yake ya Melanti Chiefs ilipokuwa ikicheza nyumbani dhidi ya Black Mamba.

Awali kiungo huyo alilazimishwa kupumzika kucheza soka kwa muda wakati akiwa klabu ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini mwaka 2016 baada ya kugundulika kuwa na matatizo ya kiafya hasa sehemu ya moyo.

Mshambuliaji wa Yanga, Tambwe amethibitisha taarifa hizo za kifo cha Faty baada ya Shirikisho la Soka Burundi kuwajulisha kundi la wachezaji wa taifa hilo.

"Ni kweli Faty amefariki jioni leo hii tumejulishwa muda si mrefu, imetusikitisha sana unajua ndiyo alianza kucheza baada ya kuambiwa apumzike kwa muda mrefu,” ameelezea Tambwe.

Faty alikuwepo katika kikosi cha Burundi ‘Intamba m'Urugamba’ kilichofuzu Fainali za Mataifa Afrika kilichotoa sare dhidi ya Gabon na kufuzu kwa mara ya kwanza fainali hizo.

Advertisement

Advertisement