Ujanja wa Wacameroon wanusa nusu fainali, waichapa Guinea 2-0

Muktasari:

Fainali za vijana chini ya miaka 17 AFCON zinaendelea kutimua vumbi jijini Dar es Salaam tangu Aprili 14 na tamati itakuwa Aprili 28.

Dar es Salaam. Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Guinea, umemfanya Kocha Mkuu wa Cameroon, Thomas Libih amesema alijua ubora mapungufu ya wapinzani wao ndiyo maana wameibuka na ushindi huo.

Cameroon wameibuka na ushindi katika fainali za AFCON zinazoendelea jijini Dar es Salaam na mchezo huo ulipigwa Uwanja wa Chamazi kuanzia 8:00 mchana.

Mabao yao yalifungwa na Steve Mvoue dakika ya 41 na Leonel Wamba alimalizia la pili dakika ya 71.

Amesema, Guinea ni timu nzuri na walijua watapata ushindi na haikuwa rahisi kupata matokeo hayo.

"Nashukuru wa pointi tatu tulizopata. Ushindi wetu ni kwa sababu tulijua ubora na udhaifu wa wapinzani wetu kabla," alisema Libiih.

Kocha wa Guinea, Mohammed Maleah amesema anajua Cameroon ni timu nzuri katika mashindano haya walijiandaa, lakini ikawa hivyo.

"Tumefungwa ni hali ya mchezo kwa sababu kwenye soka hakuna maajabu zaidi ya maandalizi," alisema Maleah.

Amefafanua kuwa wanajiandaa kwa ajili mechi nyingine zijazo ambapo Guinea imebakisha michezo miwili dhidi ya Senegal na Morocco.