Pogba, Kante hawana viwango kucheza Madrid

Muktasari:

Fowadi huyo amesema kitu kinachofanana pia kuhusu kiungo wa Chelsea, N’Golo Kante kwamba naye hana vigezo wa kwenda kuichezea Real Madrid.

MADRID HISPANIA

UNAMKUMBUKA Iago Aspas? Yule straika wa Kihispaniola aliyechemsha kwenye Ligi Kuu England wakati alipokuwa na kikosi cha Liverpool, basi ameibuka na kudai kwamba kiungo wa Manchester United, Paul Pogba hawa viwango vya kwenda kucheza Real Madrid.

Straika huyo, Aspas, ambaye kwa sasa anakipiga katika kikosi cha Celta Vigo alisema kwamba Pogba bado hana ubora wa kihivyo wa kwenda kupata nafasi ya kucheza katika kikosi hicho cha wababe wa Santiago Bernabeu.

Siku za karibuni kumekuwa na ripoti nyingi zinazomhusisha Pogba kuwa na mpango wa kwenda Real Madrid huku kocha wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer akituhumu kwamba Los Blancos wamekuwa wakitumia vyombo vya habari kulizungumza sana suala hilo la mchezaji wake kwenda Madrid.

Fowadi huyo amesema kitu kinachofanana pia kuhusu kiungo wa Chelsea, N’Golo Kante kwamba naye hana vigezo wa kwenda kuichezea Real Madrid.

Aspas alisema hivi: “Pogba au Kante? Hapana. Hawa sio wachezaji wa Real Madrid.

“Kuna kiungo mmoja ninayempa nafasi. Pale wanaye (Dani) Ceballos, ni wa kimataifa na wanachopaswa ni kumwendeleza tu kwa sababu miaka yake ndio kwanza 21. Kama ingekuwa Thiago Alcantara wa Bayern Munich kwa mfano, hapo ningewachagua Pogba na Kante.