Full mzuka: Madogo Afcon wanaupiga usingizi hapa mwanangu

Muktasari:

Mbali na ubingwa, mataifa hayo ambayo ni Tanzania, Senegal, Cameroon, Nigeria, Angola, Uganda, Morocco na Guinea yatawania nafasi nne za kuiwakilisha Afrika kwenye fainali za Kombe la Dunia la U17 Oktoba mwaka huu nchini Brazil.

Dar es Salaam. Keshokutwa Jumapili kipenga cha Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON U17) zinazofanyika kwa mara ya kwanza nchini kitapulizwa rasmi kuanza mashindano hayo yanayoshirikisha mataifa nane ya Afrika.
Mbali na ubingwa, mataifa hayo ambayo ni Tanzania, Senegal, Cameroon, Nigeria, Angola, Uganda, Morocco na Guinea yatawania nafasi nne za kuiwakilisha Afrika kwenye fainali za Kombe la Dunia la U17 Oktoba mwaka huu nchini Brazil.
Tayari timu zote zimeshawasili nchini kwa ajili ya fainali hizo na kama ilivyo utaratibu, zimepangiwa katika hoteli mbalimbali ambazo zimekidhi vigezo vilivyowekwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Kwa mujibu wa kamati ya ndani ya maandalizi ya fainali hizo, jumla ya hoteli sita (6) zimepata fursa ya kuhudumia timu, maofisa na wageni mbalimbali watakaokuwapo nchini wakati wa mashindano hayo.

Hata hivyo, bado hoteli nyingine zitakuwa na fursa ya kuhudumia wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi, lakini makala hii inakuletea dondoo fupi za hoteli sita ambazo zimechaguliwa rasmi kupokea na kuhifadhi timu, maofisa pamoja na wageni katika kipindi chote cha mashindano.

1. Serena Hotel
Wageni: Maofisa wa CAF
Bei ya chumba kwa siku: Dola 165  - Dola 571 (Sh. 380,000  - Sh. 1.3 milioni)
Eneo: Mtaa wa Ohio, Dar es Salaam

Anuani:
P.O BOX 791
Dar es Salaam, Tanzania
Simu: (+255 22) 2212500
Faksi: (+255 22) 2113981
Barua pepe: [email protected]

2. Seascape Hotel
Wageni: Timu Nigeria na Senegal
Bei: Kuanzia Dola 100 (Sh. 231,000)
Eneo: Jangwani Beach, Africana, Mbezi Africana, Dar es Salaam

Anuani
P.O.Box: 38081 Dar es Salaam, Tanzania
 Simu: +255 22 264 7405, +255 689 101 007
Faksi: +255 22 264 7407
Barua pepe: [email protected]

2. Ledger Plaza Bahari Beach Hotel
Wageni: Timu Tanzania na Morocco
Eneo: Kunduchi Mtongani, Dar es Salaam
Bei: Kuanzia Dola 81 - Dola 255 (Sh.187,000  - Sh.589,000) 
Anuani
Simu: +255 22 555 0301

3. Holiday Inn
Wageni: Timu Angola na Guinea
Eneo: Posta Mpya, Mtaa wa Azikiwe, Dar es Salaam

Bei: Kuanzia Dola 150 (Sh. 346,000)

Anuani:
Simu: +255 222 139 250
Barua Pepe: [email protected]

4. Sea Cliff Hotel
Wageni: Maofisa CAF & FIFA
Eneo: Msasani Peninsula, Toure Drive Dar es Salaam
Bei: Kuanzia Dola 150 (Sh. 346,000)
Anuani:
Simu: +255 764 700600
Barua Pepe:  [email protected]

6. Peacock Hotel
Wageni: Timu Uganda na Cameroon
Eneo: Mtaa wa Bibi Titi Mohammed, Dar es Salaam
Bei: Kuanzia Dola 70 (Sh.162,000)
Anuani:
Simu: +255 713 559 627 /+255 222 114 071
Barua Pepe:  [email protected]