Polisi yatumia mabomu kutawanya mashabiki Uwanja Taifa

Muktasari:

Mashabiki wengi waliokuwa nje ya uwanja walisikika wakilalama juu ya ufinyu wa tiketi kiasi cha kujikuta wakizurura bila kuwa na msaada wowote

Dar es Salaam. Polisi imetumia mabomu ya machozi kutawanya mashabiki waliokuwa wamepitia uwanja wa Uhuru baada ya mageti makubwa kujaa.

Mashabiki hao walielekezwa na watu wa Selcom kutokana na mageti kujaa, lakini baada ya msongamano kuwa mkubwa iliwalazimu polisi kutumia mabomu ya machozi.

Mabomu hayo yalisaidia kutawanya mashabiki waliokuwa wamekaa uwanja uhuru kiasi cha kukimbizana na kukanyagana.

Wingi wa mashabiki ulionekana mkubwa kuliko idadi ya mapolisi ambao wamejitokeza uwanjani hapa kiasi cha kutumia mabomu ya machozi kuwatanya.

TIKETI MTIHANI

Katika upande wa tiketi kulikuwa na changamoto baada ya kujitokeza idadi kubwa ya watu huku tiketi zikiwa chache.

Mashabiki wengi waliokuwa nje ya uwanja walisikika wakilalama juu ya ufinyu wa tiketi kiasi cha kujikuta wakizurura bila kuwa na msaada wowote.