Kumbe Manchester United iliandaa helikopta kwa ajili ya Bale

Muktasari:

Bale kwa sasa anakipiga kwenye kikosi cha Los Blancos, lakini bado anahusishwa na mpango wa kwenda kujiunga na Man United ambapo dili hilo linaweza kufanyika mwishoni mwa msimu

London, England. Aliyekuwa kocha wa Manchester United, David Moyes amesema walishaandaa hadi helikopta ya kwenda kumbeba supastaa Gareth Bale waliyekaribia kabisa kumsajili mwaka 2013.
Moyes amefichua namna Man United walivyokuwa wamekaribia kunasa huduma ya winga huyo, ambaye baadaye aliamua kwenda kujiunga na Real Madrid akitokea Tottenham Hotspur kwa ada iliyovunja rekodi ya dunia kwa wakati huo ya Pauni 85 milioni.
"Hadi tunafika mwisho wa dirisha la usajili, muda wote tulikuwa na imani kwamba tulikuwa na nafasi ya kumnasa Gareth Bale," alisema Moyes.
"Tuliamini kwamba tungeweza kumbadili mawazo yake asiende Real Madrid kwa sababu tulikuwa tumeshafikia nusu ya mazungumzo.
"Tulimfuata na ofa ya pesa zaidi, tulijaribu kumshawishi sana, tulimfuatilia katika kila namna na tulishakuwa tumeandaa helikopta ikiwa tayari kwenda kumbeba itakapohitajika kufanya hivyo."
Bale kwa sasa anakipiga kwenye kikosi cha Los Blancos, lakini bado anahusishwa na mpango wa kwenda kujiunga na Man United ambapo dili hilo linaweza kufanyika mwishoni mwa msimu.